Dar es Salaam. Moto umezuka
kwenye ghala la kuhifadhia dawa za binadamu ambalo pia ni Hifadhi ya
Taifa ya Viinilishe ambalo linamilikiwa na Philips Pharmaceuticals,
lililopo eneo la Vingunguti na kuteketeza mali zilizokuwemo humo.
Tukio hilo limetokea jana saa 9 alasiri na kuzua hofu kubwa wafanyakazi katika majengo ya jirani na wapita njia.
Hofu kubwa zaidi katika eneo hilo ilitanda hasa kufuatia ghala hilo kuwa karibu na Kituo cha Mafuta cha Victoria.
“Mafundi walikuwa wakifanyakazi juu ya paa mara
tukaona moto unazuka,” alisema mmoja wa mashuhuda ambaye alijitambulisha
kwa jina la Ramadhani Lugano mfanyakazi wa karakarana mojawapo jirani
na ghala hilo.
Aliongeza: “Hatufahamu sababu, lakini juu ya ghala
kulikuwa na mafundi wakiendelea na kazi, na ndiko moto ulipoanzia kabla
ya kusambaa sehemu zingine za ghala hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki na
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi walifika eneo la
tukio muda mfupi baadaye.
“Chanzo inawezekana ikawa hitilafu ya umeme, kwani moto ulianza katika paa ambako mafundi walikuwa wakifanya kazi,” alisema
Vikosi vya kupambana na moto vilifika mara moja
eneo la tukio na kuanza kazi ya kuuzima moto huo.Alisema kuwa moto
ulidhibitiwa kwa kiasi kikubwa na mkazo ulikuwa kuhakikisha haufiki
katika kituo cha mafuta cha Victoria kuepusha madhara makubwa.
“Zimatoto wamefanya kazi kubwa kuudhibiti moto
kuendelea kuteketeza ghala na mali zilizopo ndani. Hii ni kwa sababu
walifika eneo la tukio mapema na kuanza kuudhibiti moto huo,” alisema
zaidi.
“Hatujui viinilishe kiasi gani vimeharibiwa na moto na hata hasara ya jumla,” alisema Sadiki na kuongeza:
“Viinilishe ambavyo vimeteketezwa ni vile ambavyo vipo katika mpango uliozinduliwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete.
Alisema Rais Kikwete, hivi karibuni alizindua
mpango wa kuwekwa viinilishe katika vyakula, na ghala hilo liliteuliwa
kuhifadhi viinilishe hivyo. Katika eneo la tukio kulikuwa na ulinzi huku, askari wa vikosi vya
ukoaji wakihaha kuzima moto huo. Taarifa za baadaye zilithibitisha kuwa
hakukuwa na mtu yeyote aliyepata madhara.
credit, mwananchi
credit, mwananchi
0 comments:
Post a Comment