Shirika la Viwango (TBS)
Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kuzikamata bidhaa hizo katika masoko ya manispaa ya Ilala, Afisa Viwango wa TBS, Paul Manyilika, alisema zoezi hilo ni endelevu kutokana na nguo hizo kuwa na madhara makubwa kwa binadamu.
Alisema kwa sasa mikakati yao ni kuhakikisha nguo hizo haziingii sokoni na kwamba wataweka ulinzi wa kutosha kwenye bandari bubu ili zisiingizwe nchini.
Alisema kwa sasa wamejipanga kuelekea katika masoko ya mkoani ili kuzikamata bidhaa hizo na kwamba wataanza na Arusha, Kilimanjaro na Mbeya. Naye Afisa Habari wa TBS, Roida Andusamile alisema watu waliokuwa wakiuza nguo hizo hawajakamatwa kwani walikimbia na kuziacha bidhaa zao. Alisema lengo lao pia ni kuwakata watu wanaojihusisha na biashara ya nguo za ndani za mitumba waweze kueleza wanakozipata ili wasambazaji wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment