Dar es Salaam. Tanzania jana
ilifanya kweli katika mashindano ya Afrika Mashariki na Kati ya tenisi
baada ya kuibuka na ushindi katika michezo ya vijana wenye miaka 14 na
16 kwenye viwanja Dar es Salaam Gymkhana.
Katika mashindano hayo, Watanzania Omary Sulle na Tumaini Martin waliibuka na ushindi.
Katika mashindano ya vijana wa umri wa miaka 14,
Omary Sulle alikuwa bingwa baada ya kumshinda Kabura Shakuru kutoka
Burundi kwa 6-2,6-3.
Mtanzania huyo anayesoma katika chuo cha tenisi nchini Burundi, aliingia fainali baada ya kumshinda Jonathan Mugisha 6-4,6-2.
Katika mashindano ya vijana wenye umri wa miaka
16, Tumain Martin alikuwa bingwa baada ya kumshinda Emmanuel Mallya pia
wa Tanzania kwa 6-2,4-6,6-4, ambapo katika nusu fainali Martin
alimshinda Ernest Habiyambere kutoka Rwanda kwa 6-1,7-5.
Kwa upande wa umri wa 12, Shah Kean kutoka Kenya alimshinda Ryan Randiek pia kutoka Kenya kwa 6-4,6-3.
Kwa wasichana miaka 16, Sara Kassim kutoka
Ethiopia alimshinda Akutoyi kutoka Kenya 6-4,6-3 na upande wa miaka 14
wasichana Nyokuru Asha kutoka Burundi alimshinda Naihimana Sada pia wa
Burundi kwa 7-5,6-1.
0 comments:
Post a Comment