pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

"It is not fair" mume ampiga vibaya mkewe baada ya kumwomba hela ya Dawa..!

Picha sio ya Tukio husika
Sumbawanga. Mwanamke mmoja mkazi wa Kijiji cha Mnyamasi, Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, Tatu Mihambo (20) amejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa na mumewe kwa fimbo na kisha kumwagiwa maji ya moto kwa madai ya kukasirishwa na kitendo cha kumuomba fedha ya matumizi.
Taarifa zilizopatikana zinaeleza kwamba, tukio hilo la ukatili wa kijinsia lilitokea juzi, saa 7 mchana, nyumbani kwa wanandoa hao kijiini hapo ambapo inadaiwa kuwa mwanamke huyo ni mke wa pili wa Juma Masasila aliyefanya kitendo hicho.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema siku ya tukio, Tatu alimtaarifu mumewe kuwa anajisikia kuumwa na kichwa hivyo alimuomba fedha ili akatafute dawa ya kupunguza maumivu.
Alisema kitendo hicho kilimkera mumewe na ndipo alipomueleza mkewe kuwa, ukoo wao huwa hawatumii dawa zinazouzwa kwenye maduka ya dawa na kumtaka akatafute dawa za miti shamba sambamba na kwenda haraka shambani kufukuza Tumbili wasile mazao.
Kidavashari alieleza kuwa Tatu alitii agizo hilo la mumewe la kwenda shamba kulinda mazao huku kichwa kikiendelea kumuuma.
Alieleza ilipofika saa 12.00 jioni, Tatu alirejea nyumbani huku akiwa na maumivu makali ya kichwa na alimsisitiza mume wake aende dukani kumnunulia dawa.
Badala ya mumewe kwenda kumtafutia dawa dukani alianza kumshutumu mkewe kuhusu upotevu wa panga.
Mkewe alikataa madai hayo na majibu hayo yalimkera mtuhumiwa aliyeanza kumshambulia mkewe kwa fimbo na kisha alichukua maji ya moto na kumumwagia mkononi na kwenye makalio .
Inaelezwa kuwa Tatu aliendelea kuugulia maumivu yake akiwa nyumbani bila kupata matibabu yoyote na vidonda kuanza kutoa harufu ndipo mume aliposhtuka na kumpeleka kijiji cha jirani cha Lwafi kwa ajili ya matibabu ya dawa za kienyeji.
Inasemekana walipofika kijijini hapo watu walishtushwa na hali ya mgonjwa huyo na kumuhoji mtuhumiwa aliyewadanganya kuwa alianguka kwenye mti wa ukwaju, lakini mkewe aliwaeleza ukweli na ndipo walipoanza kumshambulia.
Kamanda Kidavashari alisema, baada ya muda taarifa ziliwafikia polisi na walifika katika eneo hilo na kumkamata mtuhumiwa huyo na walimchukua Tatu na kumkimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambako amelazwa akiwa anaendelea na matibabu huku hali yake ikiwa mbaya na anaongea kwa tabu
CREDIT, GUMZO

0 comments:

Post a Comment