Saudi Arabia imefanya mashambulizi mapya ya anga nchini Yemen na
kupiga maeneo kadhaa ya nchi hiyo maskini ukiwemo mji mkuu, San'aa.
Ripoti zimeeleza kuwa, ndege za kivita za Saudi Arabia zimeushambulia
mji wa San'aa na kuwauwa watu 23 wakiwemo wanawake tisa na watoto
wawili. Ndege za kivita za Saudia pia zimeushambulia mji wa Haradh
katika mkoa wa kaskazini mwa Yemen wa Hajjar karibu na mpaka wa nchi
hiyo na Saudi Arabia. Ndege hizo pia zimefanya mashambulizi sita katika
wilaya ya Jidan katika mkoa wa Ma'rib katikati mwa Yemen. Ripoti
zimeeleza pia kuwa magari matatu ya raia yameshambuliwa na ndege za
kivita za Saudia katika wilaya ya Hazm katika mkoa wa al Jawf huko
kaskazini magharibi mwa Yemen.
Wakati huo huo Maelfu ya raia wa Yemen wamefanya maandamano makubwa leo mjini San'aa na katika miji mingine ya nchi hiyo wakipinga mashambulizi ya kinyama yanayoendelea kufanywa na jeshi la Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya watu wa nchi hiyo.
Maelfu ya raia wasio na hatia wa Yemen wameuawa na malaki ya wengine kuwa wakimbizi katokana na mashambulizi hayo ya Saudia

0 comments:
Post a Comment