
Waswiswi wameamua kwenye kura
ya maoni kwamba wanataka kuweka kiwango cha wageni wanaoingia, yaani ni
kama kutaka kutoka katika makubaliano yanayoruhusu raia wa Umoja wa
Ulaya kuingia na kufanya kazi nchini humo.
Kura ya maoni iliyopendekeza kwamba idadi ya wahamiaji iwe na kikomo, ilipita kwa asili-mia-50-pointi-tano.Kinataka kuweka idadi maalumu ya wafanyakazi wa kigeni.
Serikali na wafanya biashara wanasema wahamiaji wananufaisha uchumi wa nchi.
Halmashauri ya Umoja wa Ulaya imesema imesikitishwa na matokeo hayo, lakini ilisema itachunguza vipi matokeo hayo yataathiri uhusiano baina ya Umoja wa Ulaya na Uswiswi.
Tangu kufikia makubaliano na Umoja wa Ulaya, wahamiaji 80,000 wamekuwa wakiingia Uswiswi kila mwaka - nchi yenye wakaazi milioni nane tu.
0 comments:
Post a Comment