Rais Vladmir Putin wa Urusi
amefungua rasmi mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi katika mji wa
utalii wa Socchi katika sherehe iliofana.
Waliokuwa wanariadha mashuhuri nchini Urusi
waliubeba mwenge wa Olimpiki kabla ya kuwashwa na aliyekuwa mlinda lango
wa mchezo ya magongo Vladislav Tretiak pamoja na Mchoraji wa barafu
Irina Rodnina.Awali mashabiki waliongozwa katika sherehe iliofana kuhusu historia ya Urusi na mchango wake ulimwenguni.
Katika siku 16 zijazo,karibia wanariadha 3000 watashiriki katika michezo 98 tofauti katika mashindano hayo yaliodaiwa kugharimu takriban dola billioni 50.
bbc
0 comments:
Post a Comment