Waziri wa Uhamiaji wa
Uingereza, Mark Harper, amejiuzulu baada ya kujulikana kuwa amemuajiri
mtu asiyekuwa na kibali cha kubaki nchini.
Alieleza kuwa alidanganywa na mwanamke mmoja aliyemuonesha nyaraka za bandia, alipomuajiri kusafisha nyumba yake.Bwana Harper alisema kwa sababu alichangia kupitisha bungeni sheria ngumu kuhusu uhamiaji, alihisi inambidi kuwajibika zaidi kushinda wengine.
Chama cha Conservative kimeahidi kupunguza idadi ya watu wanaohamia Uingereza kutoka malaki na kuwa elfu kadha tu.
0 comments:
Post a Comment