
Ndege hii ilikuwa imewabeba jamaa na familia za wanajeshi
Ndege ya usafiri wa jeshi nchini Algeria imeanguka ikiwa imebeba zaidi ya watu 100.
Redio ya taifa inasema ndege hiyo aina ya
Hercules C-130 ilianguka katika eneo la milima katika jimbo la Oum El
Bouaghi kusini mashariki mwa mji mkuu , Algiers na ilikuwa imewabeba
abiria 103 wakiwemo wafanyakazi wa ndege.Miili 71 ya watoto na wanawake imepatikana katika eneo la ajali
Taarifa zinasema kuwa wamepata mtu mmoja aliyenusurika huku waokozi wakiendelea kutafuta manusura zaidi.
Duru zinasema kuwa upepo mkali pamoja na hali mbaya ya anga ndiyo huenda ilisababisha ndege hiyo kuanguka.
Jeshi halijatoa taarifa yoyote mpaka sasa.
Ajali hii inasemekana kuwa mbaya zaidi kushuhudiwa katika mwongo mmoja na ya tatu ikihusisha ndege ya jeshi.
Ndege nyingine ya kampuni ya Air Algerie Boeing 737, ilianguka punde baada ya kuruka kutoka mjini Tamanrasset mnamo mwaka 2003,na mtu mmoja pekee ndiye alinusurika.
0 comments:
Post a Comment