KLABU
ya Arsenal imeaga michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya sare ya
1-1 na mabingwa watetezi usiku huu Uwanja wa Allianz Arena mjini Munich.
Timu
ya Arsene Wenger iliyofungwa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza Uwanja
wa Emirates sasa inahamia kwenye Europa League baada ya kipigo ha jumla
cha mabao 3-1.
Bastian Schweinsteiger alitangulia kuifungia Bayern dakika ya 54 na Lukas Podolski akaisawazishia Arsenal dakika ya 57.
Oxlade-Chamberlain akienda chini baada ya kukutana na Bastian Schweinsteiger
Frank Ribery akiwatoka Oxlade-Chamberlain (kulia) na Santi Cazorla (kushoto)
Wachezaji wa Bayern wakisherehekea baada ya kuitoa Arsenal
MADRID
AC
MILAN imeungana na Arsenal kuipa mkono wa kwaheri michuano ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya baada ya kutandikwa mabao 4-1 na Atletico Madrid usiku
huu Uwanja wa Vicente Calderon katika mchezo wa marudiano Hatua ya 16
Bora.
Milan
sasa inaaga kwa kipigo cha jumla cha 5-1, baada ya awali kufungwa 1-0
nyumbani. Diego Costa alitangulia kuifungia Atletico dakika ya tatu pasi
ya Koke, kabla ya Ricardo Kaka kuisawazishia Milan dakika ya 27 pasi ya
Poli.
Milan
ikatepeta na kuongezwa mabao matatu wafungaji Turan dakika ya 40, pasi
ya Raul Garcia, aliyefunga la tatu dakika ya 71 kwa pasi ya Gabi na
Diego Costa akakamilisha safari ya Atletico kuelekea Nane Bora ya Ligi
ya Mabingwa kwa bao zuri dakika ya 85 pasi ya Sosa.
0 comments:
Post a Comment