Wizara
ya Fedha kupitia Naibu wake Waziri wa fedha Mh. Mwigulu Nchemba
wametangaza uamuzi wa kufuta malipo ya Wabunge waliosusia vikao vya
mchakato wa Katiba vinavyoendelea Dodoma.
Uamuzi huu umetangazwa ikiwa ni siku ya pili tangu Wajumbe wa Bunge
la Katiba Kutoka UKAWA wasusie Shughuli za Bunge la Katiba kwa Madai
wamechoka matusi na Kuburuzwa kwenye Bunge hilo.
Hii leo Naibu waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Nchemba ambaye kwa Sasa
anakaimu Kuwa Waziri wa Fedha tangu April 10 20014 baada ya Waziri wa
Fedha kupata safari ya kikazi nchini Marekani,amefuta Malipo ya wabunge
waliosusia Mchakato huo wa Katiba.
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ameagiza Benki zote kurudisha Cheque za
Malipo ya Posho na seating allowance ambazo zilipelekwa Bungeni April 16
ili ziwekwe kwenye akaunti binafsi za Wabunge ikiwa ni Malipo ya Mpaka
April 30.
0 comments:
Post a Comment