pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Katibu Mkuu FIFA kutua Dar

Katibu Mkuu Jerome Valcke, FIFA kutua Dar 

KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Jerome Valcke, anatarajiwa kuwasili nchini Mei Mosi mwaka huu ambako atafungua semina ya mawasiliano itakayoshirikisha viongozi wa vyama wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, alisema Valcke ambaye hii ni mara yake ya kwanza kuja Tanzania, atafuatana na maofisa wengine saba wa FIFA.
Malinzi alisema semina hiyo iliyoandaliwa na FIFA, itafanyika kwa siku mbili, ambapo vilevile Valcke atapata fursa ya kuzungumza na waandishi wa habari wa ndani na wa kimataifa.
Rais huyo wa TFF, aliongeza kuwa washiriki wa semina hiyo ni marais, makatibu wakuu na wakuu wa mawasiliano wa wanachama 12 wa Cecafa, ambao ni Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda.
Naye Mwenyekiti wa Cecafa, Leodegar Tenga, ambaye alifuatana na Katibu Mkuu wake, Nicholas Musonye, alimshukuru Rais wa TFF kwa kukubali kuwa mwenyeji wa semina hiyo, kwani itasaidia katika maendeleo ya mpira wa miguu katika ukanda huu.
freemedia

0 comments:

Post a Comment