KABLA YA TUKIO BAADA YA TUKIO
Mwanafunzi ambaye amefahamika kwa jina moja la LEMA Alikua akisoma mwaka
wa 4 kozi ya sheria katika chuo kikuu kishiriki cha Mt.Augustino Tawi
la Iringa (Ruaha University College-RUCO).
Taarifa za awali zilizotufikia zimeeleza kuwamnamo tarehe 24.06.2014
mwanafunzi huyo alikua ametoka kuangalia michuano ya kombe la dunia na
akiwa amelewa akawa anatafuta chakula cha jioni na ilikua majira ya saa 5
Usiku, Mwanafunzi huyo aliingia kwenye mgahawa ambao biashara ilikua
imefungwa kwa muda huo lakini ndani kulikuwapo na Binti ambaye alianza
kupiga kelele kwa kudhani alikua mwizi. Na kwakua eneo hilo mkulikuwa na
mlinzi(Mmasai) ndiye aliyeanza kumshambulia mwanafunzi huyo.
Baada ya tukio hilo wakatokea watu (2) waliojitambulisha kuwani askari
wakaamuru mwanafunzi huyo asipigwe kwa madai ya kumfikisha kituoni.
Lakini baada ya mwendo mfupi kuelekea kituoni wananchi wenye hasira kali
walimchukua kijana huyo kinguvu na kwenda kumchoma moto.
Mpaka sasa Kijana huyo amelazwa katika wodi ya watu mahututi (ICU) katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa.
0 comments:
Post a Comment