Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango, Dkt. Philip I. Mpango (wa tatu kushoto) akipata maelezo kuhusu
Mradi wa Chuma Liganga kutoka kwa Nie Zhiyan (kulia), ambae ni Makamu Afisa Muendeshaji
Mkuu wa Tanzania China International Mineral Resources Ltd (TCIMRL). Hili ni eneo ambalo kiwanda cha chuma chenye uwezo
wa kuzalisha tani milioni moja kwa mwaka kitajengwa. Kutoka kushoto, wengine ni
Bw. Ramson Mwilangali, Kaimu Mkurugenzi wa Viwanda Mama - NDC , Bw. Erasmus
Masumbuko, Mchumi - Tume ya Mipango, Bw. Maduka Kessy, Naibu Katibu Mtendaji
Tume ya Mipango, anaeshughulikia Sekta za Uzalishaji, Bw. Israel Mkojera Makamu
Meneja Utawala - TCIMRL, Bi. Florence Mwanry Naibu Katibu Mtendaji Tume ya
Mipango anaeshughulika na Huduma za Jamii na Idadi ya Watu na Bw. Mlingi E.
Mkucha, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NDC.
Kilima
chenye madini Ya chuma, ambapo shughuli ya uchimbaji wa chuma unategemea
kuanza kutekelezwa. Uzalishaji wa chuma unatarajiwa kuanza mwaka 2016.
Viongozi
na Maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwa katika eneo ambalo
uchimbaji wa chuma utatekelezwa. Pamoja nao ni Viongozi kutoka National
Development Corporation (NDC) na Tanzania China International Mineral Resources
Ltd. Nyuma ni kilima ambacho kimejaa utajiri wa mawe yenye madini ya chuma
ambapo jiwe linakadiriwa kuwa na chuma kwa 52%.
Viongozi na maofisa kutoka Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango (ORTM), National Development Corporation (NDC) na
Tanzania China International Mineral Resources Ltd (TCIMR) wakiwa pamoja na viongozi
wa kijiji cha Mundindi ambapo ni eneo ambalo Mradi wa Uchimbaji wa Chuma
utatekelezwa. Viongozi hawa pamoja na wanakijiji wameonyesha ushirikiano mzuri
na mwekezaji katika kufanikisha utekelezaji wa mradi.
Timu
kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakipata maelezo kutoka kwa wataalam wa
kampuni ya Tanzania China International Mineral Resources Ltd kuhusu Iron Ore Samples zilizopatikana wakati
wa utafiti kuhusu wingi na ubora wa chuma kitakachopatikana katika eneo la
Liganga.
Katibu
Mtendaji Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Dkt. Philip I. Mpango (aliyesimama)
akiongea na Viongozi wa Kijiji cha Mundindi pamoja na viongozi na wataalam wa
kampuni ya Tanzania China International Mineral Resorces Ltd.
Picha na: Thomas Nyindo.
0 comments:
Post a Comment