WATU wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha aina ya
Short gun wamepora kiasi cha Sh milioni 20 kutoka kwa mtumishi wa duka
la kubadilishia fedha za kigeni la Northern Bureau de Change na kumpiga
risasi mtu mmoja na kufa papo hapo.
Tukio hilo lililotokea saa 3.30 asubuhi jana katika duka hilo mali ya
Hotel ya Impala lililopo mtaa wa Maeda katikati ya Jiji la Arusha.
Watuhumiwa hao wakiwa na pikipiki waliondoka eneo hilo kupitia
barabara ya zamani ya Moshi kuelekea Kijenge mara baada ya tukio hilo.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, walisema majambazi hao
walifika eneo hilo na pikipiki na kuegesha eneo zinapoegeshwa teksi na
kumsubiri mtumishi wa duka hilo aliyetambuliwa kwa jina moja la Mama
Msuya ambaye jana aliingia kazini na usafiri mwingine tofauti na
unaojulikana.
Mmoja wa watu hao ambaye hakuwa tayari kusema jina lake, aliendelea
kusema mara baada mtumishi huyo kufika akiwa na mfuko mweusi wenye kiasi
hicho cha fedha, ghafla alivamiwa mlangoni wakati akiwa anafungua duka
hilo na kuanza kunyang’anyana mfuko huo.
Alisema wakati jambazi huyo mmoja akipambana na Mama Msuya na kumpiga
kibao huku akimuamurisha kutoa fuko hilo la fedha, mama huyo alipiga
kelele kuomba msaada na madereva teksi walikwenda haraka kutaka
kumsaidia.
Lakini hali ilibadilika baada ya jambazi mwingine aliyebaki katika
pikipiki kuteremka na silaha na kwenda kumpiga risasi mmoja wa watu
aliyetaka kwenda kutoa msaada aliyetambuliwa kwa jina mmoja la Mmasi
ambaye ni mchimba madini ya tanzanite na kufa papo hapo.
Mtoa habari huyo alisema Mmasi alikuwa ametoka kusali katika Kanisa
la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mjini Kati na
alikwenda kununua magazeti eneo hilo na alipoona mama akipiga kelele
kuomba msaada, alikwenda kwa lengo la kumuokoa lakini kabla ya kufika
alipigwa risasi ubavuni na kufa papo hapo na jambazi aliyekuwa pembeni
na Toyo
0 comments:
Post a Comment