Inaripotiwa kuwa China imetuma
silaha zenye thamani ya dola milioni 38 nchini Sudan Kusini licha ya
nchi hiyo kukabiliwa na mzozo ambao huenda utaitumbukiza katika baa la
njaa.
Nyaraka zilizogunduliwa na wataalamu wa masuala
ya ulinzi zinaonyesha kuwa makombora, bunduki za rashasha na risasi
viliwasili nchini Sudan Kusini mwezi uliopita kupitia bandari ya
Mombasa nchini Kenya.Kwingineko, muungano wa ulaya umewawekea vikwazo viongozi na kupiga tanji mali ya wakuu wa kijeshi wa nchi hiyo kwa tuhuma za kukiuka makubaliano ya kusitisha vita ambayo yangeleta mazingira ya amani na kuziia mauaji ya maelfu ya wanachi.
Marekani imechukua hatua sawa na hizo dhidi ya viongozi kutoka pande zinazozozana.
Vita vilizuka mjini Juba Disemba mwaka jana kati ya serikali na wapiganaji wa aliyekuwa makamu wa Rais Riek Machar.
Mgogoro huo bila shaka umetonesha kidonda katika taifa hilo changa zaidi duniani tangu kujitawala mwaka 2011.
0 comments:
Post a Comment