Brigedi za Izzuddin al Qassam, tawi la kijeshi la harakati ya
Hamas limesema kuwa, wanamapambano wa Kipalestina wameshawaangamiza
wanajeshi 32 wa utawala wa Kizayuni wa Israel tangu jana Jumamosi. Duru
za kijeshi za Hamas zimesema kuwa, wanajeshi wa Israel waliojeruhiwa
katika mapigano na wanamapambano wa Palestina wamepelekwa hospitalini,
huku kamanda wa kikosi maalumu cha makomandoo wa Israel cha Golan akiwa
miongoni mwa waliojeruhiwa. Utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa ukitoa
taarifa za kutatanisha kuhusu idadi ya wanajeshi wake waliouawa, mara
inakiri ni wanajeshi wawili, mara ni wanajeshi saba, na pia kuna taarifa
kuwa Israel imekiri kuuawa wanajeshi wake wanane. Wanamapambano wa
Palestina aidha wameshambulia kwa makombora vifaru sita vya utawala wa
Kizayuni wa Israel. Vile vile karibu makombora 2000 ya wanapambano wa
Palestina yameshavurumishwa kwenye miji ya Wazayuni kama vile Tel Aviv,
Demona, Eshkol na Be'er Sheva tangu Israel ilipoanza kuishambulia Ghaza
siku 13 zilizopita. Aidha mtandao wa al Aqsa umeripoti kuwa utawala wa
Kizayuni umepata hasara kubwa pia katika mapigano yanayoendelea tangu
leo asubuhi. Wakati huo huo maandamano ya kupinga jinai za Israel
yameshadidi katika kona mbalimbali za dunia zikiwemo za nchi za Ulaya
Magharibi pamoja na Marekani.
0 comments:
Post a Comment