Huenda sio wachezaji wageni ,
lakini michuano ya kombe la dunia Brazil iliwaleta wachezaji hao kwa
sura tofauti sana kwa mashabiki wa soka duniani.
Hata cha muhimu zaidi ni kwa mawakala wa
wachezaji hao, wachezaji wao walipata kuvutia vilabu ambazo bila shaka
ni vilabu vyenye thamani ya mamilioni ya dola kuvutiwa na talanta zao.Hawa ni wachezaji watano waliokuwa na mvuto wa kipekee na ambao walivutia vilabu ambavyo huenda wakasaini mikataba nao.
James Rodriguez
Mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 23, aliingiza mabao sita katika mechi tano na kufikisha klabu yake katika robo fainali kabla ya kushindwa na Brazil
Rodriguez alihamia Monaco kutoka Porto mwaka jana lakini mchezo wake ulikuwa wa kufana Brazil, hasa katika mechi yao dhidi na Uruguay.
Mechi hiyo, ilimuweka machoni mwa vilabu vikubwa Ulaya hali ambayo bila shaka imepandisha thamani yake kutoka pauni milioni 38.5.
Toni Kroos
Mchezaji huyu anaonekana kuwa tayari kuondoka ligi ya Bundesliga.
Alivyocheza katika mecho zote sana imemfanya kusakwa na Real Madrid.
Kroos anayechezea Bayern Munich, aliingiza mabao mawili katika ushindi wa mabao saba dhidi ya Brazil na alionekana kusaidia sana wenzake katika kuingiza mabao.
Mchezaji mwenzake kiungo cha kati, Sami Khedira, huenda akamtengezea nafasi katika klabu ya Real huku ripoti zikisema yeye anaonekana kuelekea Arsenal.
Paul Pogba
Alitajwa kama mchezaji mwenye umri mdogo katika kombe la dunia na kupata sifa kedekede wakati wote wa mashindano baada ya kusaidia timu yake kufika robo fainali ambapo walichabangwa na mabingwa Ujerumani.
Pogba mwenye umri wa miaka 21, aliingiza bao lake la kwanza dhidi ya Nigeria katika awamu ya timu bora kumi na sita na atakuwa katika msitari wa mbele wakati Deschamps ikipanga kuwa mwenyeji wa kombe la mabingwa wa ulaya miaka miwili ijayo.
Lakini mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United, huenda akarejea nyumbani hivi karibuni kwani klabu ya Paris St-Germain inamuotea.
Xherdan Shaqiri
Amebandikwa jina la Alpine Messi, kama jina lake la utani.
Mchezaji huyu raia wa Uswizi ametajwa kama nambari moja kuingia Liverpool huku klabu hiyo ikitafuta mchezaji atakayejaza nafasi ya Luis Suarez.
Mchezaji huyu wa Bayern Munich, aliingiza bao la pekee kwa mguu wake wa kushoto katika kombe hilo walipokuwa wanacheza dhidi ya Honduras, na alitajwa mchezaji bora wa mechi mara mbili.
Hii ni baada ya kusaida timu yake kufika awamu ya kumi na sita bora dhidi ya Argentina.
Guillermo Ochoa
Raia wa Mexico, alicheza vyema sana na vilabu vimeonekana kumuotea sana vikitafuta kipa mpya.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, alifanikiwa kutajwa kama mchezaji bora zaidi alipoinyima Brazil fursa katika awamu ya makundi kabla ya kung'olewa makali na vijana wa Louis van Gaal.
Timu hiyo iliondoka katika awamu ya makundi kumi na sita bora lakini Ochoa alisemekana kuwa mchezaji bora zaidi katika mechi yao ya mwisho.
Anajiunga na Manuel Neuer, Tim Howard naKeylor Navas - ambaye ana mvuto wake kwa vilabu baada ya mchezo wa kufana wa Costa Rica, kama kipa bora zaidi wa michuano ya kombe la dunia.
0 comments:
Post a Comment