Kumekuwa na
maoni tofauti kuhusiana na video ya ‘Mdogo mdogo’ ya Diamond Platnumz
iliyotoka Jumatatu ya wiki hii. Wapo ambao wamefurahishwa na story
iliyoko kwenye video hiyo na wengine ambao hawajaiunga mkono moja kwa
moja kutokana na kila mmoja kuwa na sababu tofauti hali ambayo imeleta
mabishano mengi katika comments za youtube na kwingine.
Lakini
inawezekana wengi ama wote hatujui maana halisi ya story iliyoko kwenye
video hiyo na sababu za Diamond na timu yake kuamua kuifanya hivyo
ilivyo.
Diamond amefunguka jinsi story ya video hiyo ilivyozaliwa na script kuandikwa:
“Ujumbe
ulikuwa kwamba mapenzi yanakuwa hayachagui rangi wala kabila na kuutoa
ubaguzi kama mtoto flani labda muhindi hawezi kuolewa na mswahili au
mzungu, mswahili hawezi kumuoa muhindi au mzungu au mchina no no no…haya
ni mapenzi na wote mkiridhiana yaendane yakubalike tu. So hiyo ilikuwa
message, lakini pia nikaamua kuifanya kisehemu mbili tofauti tofauti ili
pia kutokupoteza culture halisi ya kitanzania. Ndio maana utaona kuna
character moja ndo naigiza mimi kijijini kabisa kama Tarzan yaani kama
mtu wa kijijini kabisa halafu yule ndio mtoto wa mfalme ambaye ndio
ananipenda mimi hapa.” Amesema Diamond kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM.
Diamond
pia amemtaja director maarufu wa bongo movie marehemu Adam Kuambiana
kuwa ndiye mtu aliyeleta wazo la script iliyotumika kwenye video hiyo na
baadae kuongezewa chachandu na mpenzi wake Wema Sepetu.
“Script
wakati inaanza kwanza nilikuwa sasa mimi nataka kufanya kitu flani
lakini nilikuwa sijui nakianzaje…so nakumbuka that time Adam Kuambiana
alikuwa anadirect movie ya kina baby nilikua naenda kambini nakutana
naye, na baby aliniambia ni mzuri sana, nikamfata nikamwambia bana na
wimbo wangu nataka uniandikie story …akasema basi itakua vizuri nikifika
studio na nuiisikilize….akaskiliza ngoma akawa ananipa namna story
inavyotakiwa kuanza kwenda. So naweza kusema mwanzoni wakati story
inavyoanza picha hata ya kuipata story ni Kuambiana ndo alinipaso baada
ya hapo mi nikaenda nikakaa nayo nyumbani mi na baby tukakaa baby
nikamwambia Kuambiana katoa wazo kama hili unaona tulifanyeje, so
tukakaa unajua baby nae master katika maswala ya movie movie, so akakaa
akawa anaiandika hapa iwe hivi aah isiwe hivi hapa iwe hivi, baada ya
kumaliza kuiandika akaichora katika lugha ngeni tukaituma kwa director
akaitazama na akaipitisha.”
Platnumz ameongeza kuwa video hiyo imemgharimu dola elfu 32 pamoja na gharama za kusafiri yeye na timu yake hadi Afrika Kusini.
0 comments:
Post a Comment