Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, idadi ya Wapalestina waliouawa
shahidi katika mashambulizi ya kikatili yaliyofanywa na jeshi vamizi la
Israel katika eneo la Shujaiyya huko Ghaza imepindukia watu 87 na zaidi
ya 200 wengine kujeruhiwa. Shambulio la ndege za Israel dhidi ya raia
ambao wengi wao ni wanawake na watoto wadogo limefanyika katika eneo
hilo la Wapalestina baada ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni kushindwa
katika medani ya vita. Televisheni mbalimbali za kieneo na kimataifa
zimeonesha idadi kubwa ya miili ya watu ikiwa imeenea kwenye mitaa ya
eneo hilo huku maafisa wa magari ya wagonjwa wakikiri kuwa wamezidiwa na
idadi ya watu wanaosubiri huduma zao. Akiripoti kutoka katika eneo la
Shujaiya, mwandishi wa televisheni ya Press TV amesema kuwa, hakuna hata
mwanajeshi mmoja wa Kipalestina aliyekuwemo katika watu waliouliwa
kinyama na Wazayuni huko Shujaiya. Wanamapambano wa Palestina kupitia
vyombo vyao vya habari kama vile televisheni ya al Aqsa wamesema kuwa
watalipiza kisasi cha jinai hizo mpya kabisa za utawala wa Kizayuni wa
Israel. Tayari wanamapambano wa Palestina wameushambulia kwa makombora
mji wa Beyt Yam wa karibu na mji mkuu wa utawala wa Kizayuni, Tel Aviv
pamoja na mji wa Be'er Sab'i kwa makombora aina ya M75 na Sijjil 55
ikiwa ni kutekeleza ahadi zao kwa wananchi wa Palestina kuwa hawatoacha
jinai za Wazayuni zipite vivi hivi.
0 comments:
Post a Comment