RAIS
Jakaya Kikwete amesisitiza nia ya Serikali kutumia wahitimu wake wa
vyuo vikuu, kufundisha shule za msingi huku akiwaweka sawa kwa kuwaambia
kufanya hivyo si kuwashushia hadhi.
Hatua
hiyo ya walimu wenye Shahada kuanza kufundisha shule za msingi tofauti
na ilivyozoeleka, chini ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, ni
sehemu ya mageuzi makubwa, yanayotarajiwa kufanyika katika sekta ya
elimu nchini.
Rais
Kikwete alishawahi kutamka mpango huo wa kutumia wasomi wa vyuo vikuu
katika shule za msingi, kutokana na idadi kubwa ya wahitimu wa ualimu,
kutarajiwa kuwa kwenye soko la ajira.
Alisisitiza
kuwa baada ya mwaka, wahitimu wa vyuo vikuu watafundisha katika shule
hizo na kwamba kufanya hivyo si kuwashushia hadhi.
Akihutubia
wananchi mjini Mbinga, kabla ya kufungua kituo cha mabasi na barabara
ya Peramiho- Mbinga yenye urefu wa kilometa 78, Kikwete alisema barani
Ulaya, hata walimu wa shule za chekechekea wana Shahada na kwamba hicho
ni kipimo cha maendeleo.
Kwa utaratibu uliozoeleka chini ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, walimu wa shule za msingi ni wenye cheti.
Hata hivyo, kulingana na taarifa za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, wapo wanaochukua Shahada, wanaosomea kufundisha elimu ya msingi.
Hata hivyo, kulingana na taarifa za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, wapo wanaochukua Shahada, wanaosomea kufundisha elimu ya msingi.
“Wakati
umebadilika…leo utamchukua Standard Seven ( Darasa za Saba) kwenda chuo
cha ualimu? Leo Division Four (waliopata Daraja la Nne) wanakataliwa
vyuo vya ualimu,” alisema.
Alisema,
hali ya sasa ni tofauti na miaka ya nyuma kwa kuwa sasa, hata makatibu
tarafa wana Shahada. Kwa mujibu wa tamko la Serikali, kuanzia sasa
wanaosomea ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada, sharti wawe na ufaulu wa
daraja la tatu.
Aidha,
Serikali imeamua kuanzia sasa wanaojiunga na mafunzo ya Stashahada ya
Ualimu katika masomo ya Sayansi wakiwa na ufaulu wa Daraja la Kwanza,
watasomeshwa bure. Pia wenye ufaulu wa Daraja la Pili na la Tatu,
watapewa mkopo.
Shule za Kata
Akizungumzia
shule za sekondari za kata, Rais Kikwete alipongeza maendeleo ya
taaluma, kutokana na baadhi shule hizo kuwa miongoni mwa wanaofanya
vizuri katika mitihani ya taifa.
Kwa
mujibu wa Rais Kikwete, wakati shule hizo zinaanzishwa, hali ilikuwa
ngumu tofauti na sasa ambako yapo mabadliko. Alitoa takwimu kwamba kati
ya wahitimu 71,000 waliochaguliwa kuendelea na Kidato cha Tano, 20,000
wameachwa.
Katika
mkutano huo uliohudhuriwa na wanafunzi wengi wa shule za msingi na
sekondari, Rais Kikwete aliagiza ifikapo mwaka 2016, kila mwanafunzi awe
na kitabu chake.
Alisema,
serikali imeanza kutenga fedha kwa ajili hiyo, zikiwemo Sh bilioni 21
zilizotengwa katika bajeti ya mwaka huu wa fedha 2014/2015. Rais
aliagiza fedha kwa ajili ya vitabu zitengwe na azione kwa kuwa anataka
taifa lipate wataalamu wengi.
Katika
mkutano huo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenista
Mhagama alisema katika shule za msingi hivi sasa, wanafunzi watatu
wanatumia kitabu kimoja.
Kwa
mujibu wa Mhagama, kupitia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Wilaya
ya Mbinga ilikuwa ya kwanza kitaifa kwa maendeleo ya elimu.
Aliwapongeza
walimu kwa kazi nzuri, wanayofanya wilayani humo. Alibainisha kuwa
walimu 112 waliopangiwa kufundisha katika shule za msingi walikwenda, na
wengine 138 waliotakiwa kwenda kufundisha shule za sekondari,
wanaendelea na kazi.
0 comments:
Post a Comment