pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Israel ifikishwe mahakamani: Walimwengu

 Walimwengu wanataka Israel ifikishwe mahakamani

Mauaji ya umati yaliyofanywa na jeshi la Israel katika eneo la Shujaiyya, uharibifu mkubwa wa eneo al Khazaa na umwagaji damu na mauaji ya kutisha ya jeshi la utawala katili wa Israel katika kitongoji cha Bait Hanun ni sehemu ndogo ya jinai zilizofanywa na Wazayuni katika Ukanda wa Ghaza ambazo walimwengu walizishuhudia kwa macho yao kupitia viyoo vya runinga na kutazama baba au mama waliokuwa wamebeba miili iliyoraruriwa na mabomu ya watoto wao wakiomba msaada wa Umoja wa Mataifa bila kupata majibu.
Katika mashambulizi ya Israel huko Ghaza, Umoja wa Mataifa uliokuwa chini ya mashinikizo ya Marekani haukuchukua hatua yoyote ya maana ya kusitisha mashambulizi hayo ya kinyama ambayo yametajwa kuwa hayana mfano, ghairi ya kuitisha kikao kisicho rasmi kilichofanywa na Baraza Kuu la Umoja huo kuchunguza ripoti za maafisa wa ngazi za juu wa UN kuhusu vita vya Ghaza.
Katika kikao hicho Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay alisema kuwa mashambulizi yoyote yanayofanywa dhidi ya raia, nyumba, shule na hospitali ni jinai ya kivita inayopaswa kulaaniwa. Pillay alisema kuwa tume ya uchunguzi mpya wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa imetayarisha ripoti ya mashambulizi ya Israel katika eneo la Ukanda wa Ghaza na matokeo yake yatatangazwa mwezi Machi mwaka ujao.
Utendaji wa Umoja wa Mataifa katika mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Ghaza ulipendelea waziwazi na kuinga mkono Israel kiasi kwamba walimwengu sasa wanaitambua jumuiya hiyo ya kimataifa kuwa ni mshirika wa Israel na Marekani katika jinai ziliozofanyika huko Ghaza. Wapalestina wanasema kuwa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepuuza wito wa kuomba msaada wa raia wa Ukanda wa Ghaza katika kipindi chote cha mashambulizi ya kinyama ya Israel na limeshindwa hata kutoa azimio la kulaani kwa maneno jinai zilizofanywa na utawala huo. Ban Ki-moon ameyataja mashambulizi ya Israel dhidi ya shule za Umoja wa Mataifa na ofisi za umoja huo kuwa hayakubaliki na ni ukiukaji wa sheria za kimataifa na ametoa wito wa kusailiwa viongozi wa Israel kuhusu ukiukaji wa sheria za kimataifa.
Japokuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kimataifa kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza na ameyataja mauaji ya Wapalestina wanaokaribia 2000 katika mashambulizi hayo kuwa ni aibu kwa walimwengu, lakini dunia haijasahau jinsi kiongozi huyo alivyochochea zaidi moto wa hujuma ya Israel dhidi ya watu wa Ghaza wakati wa kilele cha mashambulizi hayo kwa kuipendelea na kuitetea Israel.
Kuua na kujeruhi zaidi ya watu elfu 10 na kuwalazimisha karibu watu nusu milioni kukimbia makazi na nyumba zao ni ushahidi tosha unaowathibitishia walimwengu jinai za kivita zilizofanywa na Israel huko Ghaza na kwa msingi huo walimwengu wanatarajia kuona viongozi hao wa Kizayuni wakifikishwa mahakamani. Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel Benjamin Netanyahu amewaomba wabunge wa Congresi ya Marekani kuisaidia Israel ili isifikishwe katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC). Netanyahu amewaomba washiriki wake wa Kimagharibi wazuie jaribio la aina yoyote la kuundwa tume ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza vita vya Ghaza na taathira zake na hivyo kufunika tuhuma za kufanya jinai za kivita dhidi ya Wapalestina.

0 comments:

Post a Comment