MGOGORO
wa kugombea mwili wa marehemu, Stephen Assei (52) umechukua sura mpya
baada ya askari polisi wenye silaha za moto wakiwemo askari kanzu
kusimamia zoezi la ufukuaji wa kaburi na kisha kuondoka na jeneza lenye
mwili wa marehemu.
Hatua ya ufukuaji wa kaburi hilo inatokana na mke wa ndoa wa
marehemu, Lucy Laurant kufungua kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Moshi dhidi ya Fortunata Lyimo, akidai shughuli za maziko za marehemu
mumewe zifanyike nyumbani kwake kijiji cha Mandaka.
Lucy aliiomba mahakama hiyo kutoa amri ya kufukuliwa kwa mwili wa
Marehemu, Assei aliyefariki Septemba Mosi mwaka huu na kuzikwa Agosti 8
mwaka huu katika kijiji cha Masaera kata Kilema Kusini nyumbani kwa mke
wa pili wa marehemu aliyekuwa akiishi naye kwa zaidi ya miaka 18.
Ombi hilo lililowasilishwa na wakili wa upande wa mashitaka ,Paul
Njau, mbele ya Hakimu Mkazi Munga Sabuni, iliamriwa kufukuliwa kwa
kaburi hilo na mwili kuhifadhiwa hospatali hadi Septemba 11 mwaka huu
mahakama itakapoamua ni nani mwenye haki ya kumzika marehemu.
Baada ya shughuli za kufukua kaburi kumalizika, jeneza lenye miwli wa
marehemu lilipakizwa katika gari la Polisi ,Land Rover 110,lenye namba
za usajili ,T 989 AEV na kupelekwa katika hosptali ya Kilema kwa ajili
ya kusibiri uamuzi wa mahakama.
Baada kaburi kufukuliwa, ndugu wa marehemu wakiongozwa na kiongozi wa
Ukoo aliyetambulika kwa jina la Basil Assei wamejitokeza na kumkana
mlalamikaji anayetajwa kuwa ni mke wa ndoa wa marehemu.
“Marehemu akiwa mgonjwa alisema hataki kuzikwa katika mji wake wa
zamani anataka kuzikwa katika mji huu aliojenga mwenyewe, halafu cha
kushangaza zaidi hata watoto aliozaa na marehemu wanakaa kwa huyu mke
mdogo,” alisema Basil.
Katika hali isiyo ya kawaida kaburi alilokuwa umezikwa mwili
wamarehemu Assei, liliachwa wazi huku baadhi ya wananchi
waliokuwawakishuhudia zoezi la ufukuaji wakisema kwa mila za kichaga
kunahitajika kufanyika shughuli za kimila kabla siku haijaisha.
0 comments:
Post a Comment