pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Diamond huyooo Ujerumani tena

Diamond arudi tena Ujerumani 

SIKU chache baada ya kushindwa kufanya shoo mjini Stuttgart, nchini Ujerumani, msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ ameandaa shoo nyingine nchini humo.
Shoo hiyo itafanyika katika Ukumbi wa Melody Center Septemba 20, huku akitarajiwa kusindikizwa na nyota Sentinel, ambaye ni Mjerumani anayefanya kazi nchini humo.
Kwa mujibu wa Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram, baada ya kugundua kama sio promota wake aliyesababisha kutokea kwa vurugu hizo, ameamua kuandaa shoo hiyo akiwa na lengo la kuwaomba radhi mashabiki wake.
Aliandka kuwa, shoo hiyo itaanza saa 3:00 usiku na kuendelea na haitakuwa na kiingilio hivyo basi mashabiki wametakiwa kupendeza zaidi ili waweze kupata nafasi ya kupiga picha katika ‘Red Carpet’.
“Nimegundua kama sio promota aliyesababisha kuvunjika kwa shoo yangu wiki iliyopita, hivyo nimeamua kuwaandalia shoo nyingine mashabiki wangu naomba wafike kwa wingi ili tuweze kuburudika pamoja,” aliandika nyota huyo.
Pia aliwakaribisha mashabiki wa muziki kutoka nchi za jirani kama, Norway, Uholanzi, Uswisi, Ubelgiji na Sweeden waweze kufika ili kujumuika pamoja.
Hivi karibuni Diamond alizua balaa nchini Ujerumani, baada ya kushindwa kufanya shoo yake, ambapo mashabiki waliamua kuvunja viti na mali nyingine baada ya kuchelewa kufika ukumbini.

0 comments:

Post a Comment