pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

EURO 2015: Welbeck ang'ara England ikiiifunga Uswisi

England yaifunga Uswisi, Welbeck ang'ara
England imeanza kusaka tiketi ya kucheza fainali za kombe la Ulaya kwa kuifunga Uswisi.
England imeanza harakati hizo za kucheza fainali hizo zitakazofanyika huko Ufaransa baada ya kuishindilia Uswisi mabao 2-0 usiku wa kuamkia leo.
Mshambuliaji mpya wa Arsenal, Danny Welbeck, aliibuka nyota wa kocha Roy Hodgson kwa kazi nzuri ya kutumbukiza kimiani mabao yote mawili, huku akifunga bao la pili dakika ya mwisho ya mchezo huo uliopigwa mjini Basel Uswisi.

0 comments:

Post a Comment