Fat'hi Hammad, kiongozi mwandamizi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, harakati hiyo iko tayari wakati wowote ule kukabiliana tena na uadui wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Afisa huyo wa Hamas amesema kwamba, vikosi vya muqawama na wanamapambano wa Kipalestina wako karibu zaidi na ushindi katika vita vyovyote vipya na adui. Fat'hi Hammad ameongeza kuwa, ushindi wa muqawama wa Palestina katika vita vya hivi karibuni na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza utakuwa na nafasi muhimu mno katika ramani ya njia ya kisiasa.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, viongozi wa Israel wameendelea
kukiri kwamba Hamas imepata nguvu zaidi. Hivi karibuni Avigdor Liberman,
Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Kizayuni wa Israel alikiri kuwa,
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS inazidi kuwa na
nguvu na kuungwa mkono zaidi na Wapalestina kila Israel inavyozidi
kufanya mashambulio.
0 comments:
Post a Comment