POLISI
nchini Ujerumani wamefanikiwa kumtia mbaroni promota Awin Williams
Akpomie, aliyeratibu shoo ya mwanamuziki wa Tanzania, Naseeb Abdul
‘Diamond Platinumz’ iliyokuwa ifanyike Agosti 30, mjini Stuttgart na
kushindwa kufanyika.
Shoo hiyo haikufanyika kutoka na mashabiki kuanzisha vurugu kubwa
ukumbini wakikerwa na kitendo cha Diamond kukawia kutumbuiza kwa saa
tano, vurugu ambazo zilisababisha athari kwa baadhi ya watu kuumizwa na
vitu kuharibiwa.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka nchini Ujerumani, Jeshi la
Polisi nchini humo watamchukulia hatua za kisheria ili kuwa fundisho kwa
wengine wenye tabia kama hiyo.
Katika tukio hilo, uharibifu mkubwa ulitokea ikiwemo kuvunjwa kwa
vyombo vya muziki na vitu mbalimbali na kuna habari kuwa, promota huyo
aliuhadaa utawala wa ukumbi huo wa Sindfingen kwamba angefanya African
Party na mkutano si onyesho la muziki.
Habari zinasema, vurugu hizo zimesababisha hasara inayofikia Euro
300,000 sawa na sh. Mil.600 za Kitanzania ambazo anatakiwa azilipe.
Aidha, imeelezwa Akpomie hakuwa na bima ya kulinda onyesho hilo na
ukumbi ambao ungetumiwa kwa onyesho hilo ambao ni kwa mikutano na
maonyesho ya bidhaa si masuala ya muziki.
Taarifa za kipolisi zinasema, suala hilo tayari zimepeleka ofisi ya
Sheria ya mji wa Stuttgart zilikotokea fujo hizo kwa hatua zaidi huku
polisi wakiendelea kumshikilia kwa mahojiano Akpomie kukiwa na tetezi
amekuwa akijihusisha pia na biashara haramu.
Aidha, taasisi mbali mbali na jumuiya za Wafrika nchini Ujerumani na
jirani zimelaani vikali tabia za raia huyo kuwadanganya mashabiki na
kulivunjia hadhi sifa za bara la Afrika.
0 comments:
Post a Comment