WAKAZI
wa Msangamkuu, Mtwara Mjini mkoani Mtwara na vitongoji vyake, jana
walimiminika katika pwani ya Bahari ya Hindi kumshangaa samaki aina ya
Nyangumi mwenye urefu wa futi 48 na tani zaidi ya 30.
Mbali na mshangao huo nyangumi huyo alikuwa kivutio kwa waliomwona
huku ikielezwa kwamba mara ya mwisho samaki huyo alionekana zaidi ya
miaka 25 iliyopita.
Akizungumza na Tanzania Daima, mvuvi wa samaki huyo Saidi Hassani
‘Ngassa’ alisema Septemba 3 akiwa katika shughuli zake alizivuta nyavu
na kubaini kuna uzito usio wa kawaida uliosababisha chombo chake kuvutwa
na samaki huyo.
“Baada ya kuona anaweza kuniletea shida nilimuacha samaki huyo akiwa
kwenye nyavu nilirudi nyumbani kuwaita watu wengine ili wanisaidie
kuvuta nyavu… lakini siku ya kwanza na ya pili ilishindikana hadi siku
ya tatu tulimvuta mpaka pwani,” alisema Ngassa.
Ofisa Uvivu Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Saidi Abdallah aliwataka
wakazi wa Msangamkuu kutomla samaki huyo kwa kuwa ni sumu, badala yake
watumie mafuta yake ambayo ni dawa ya misuli.
0 comments:
Post a Comment