Muigizaji wa filamu za Kiswahili, Steve Nyerere aliyekuwa Rais wa Klabu ya Bongo Movie Unity ameamua kujiuzulu nafasi hiyo.
Steve ameeleza uamuzi wake kupitia Instagram bila kutoa sababu zilizopelekea kujiuzulu kwake.
“Napenda kuwashkulu ndugu zangu wote wasaniii wenzangu kaka zangu
mama zangu rafiki zangu mimi pamoja na family yangu nimeamua kujiuzuru
uongozi wa bongo move nabaki kuwa mwanachama wa kawaida naimani
tulifurahi pamoja tukauzunika pamoja na daima tutakuwa pamoja.”
Uamuzi wa Steve Nyerere umepokelewa kwa hisia tofauti na wapenzi wa
filamu za kitanzania ambao wengine wamemtaka kutofanya hivyo huku
wakitaja ‘majungu’ na kusemwa kama chanzo cha yote.
“Khaaaaaaa asa @stevenyerere2 kujihuzur sio suluhisho la tatizo kaanza willy umefata ww sasa c kamat nzima itajiuzur!?? Why mnashindwa kukaa km wasanii mkasuluhisha penye makosa mambo yakaendelea? Majungu yapo kila sehem kusemwa kupo kila sehem @stevenyerere2 mnapoelekea bongomovie kila mtu atakaa mwenyewe wallah.” Ameandika shabiki anaetumia jina la Neyjd.
0 comments:
Post a Comment