KIFO cha mfanyabiashara
aliyeshikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Stakishari, Ukonga jijini Dar
es Salaam, Liberatus Damiani Temu (55) kilichodaiwa kilitokana na
kipigo kutoka kwa askari wa kituo hicho sasa ukweli umejulikana.
Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu, Liberatus Damiani Temu (55) anayedaiwa kufariki kiutata.
Chanzo makini kililiambia gazeti hili kuwa utata wa tukio hilo
ulianzia mbali kwani Mei, mwaka huu, marehemu alimgonga na gari mtu
mmoja anayefahamika kwa jina la Hamis Magoma na kujeruhiwa vibaya.
Mke wa marehemu, Naomi Liberatus (katikati) akihuzunika kwa kumpoteza mwenzake.
Baada ya kusababisha ajali hiyo, ilidaiwa marehemu Liberatus
alifuatilia masuala ya bima ili aweze kumlipa aliyemgonga ambaye pia
anatajwa kuwa mteja mzuri katika Baa ya Meku iliyokuwa ikimilikiwa na
marehemu.
Naomi Liberatus akiwa amezimia wakati wa mazishi.
Chanzo kinasema baada ya kutokea kwa
ajali hiyo, hali ya Magoma iliendelea kuwa mbaya hadi Agosti 22, mwaka
huu saa tano usiku marehemu alipokamatwa na kufikishwa kituoni hapo
akidaiwa kumjeruhi Magoma kwenye ajali.
Padri akiiombea roho ya marehemu ya marehemu (Liberatus Damiani Temu).
Mke wa marehemu, Naomi Liberatus
aliyezimia mara mbili wakati wa mazishi, alisema mumewe ambaye kwa
kipindi chote tangu apate ajali hiyo, alikuwa hafanyi shughuli yoyote,
alikataliwa kupewa dhamana kwa madai kuwa majeruhi (Magoma) alikuwa na
hali mbaya.
Mwili wa marehemu Liberatus Damiani Temu ukichukuliwa kwenye gari kwa ajili ya mazishi.
Kuhusu hatua nyingine ilidaiwa kuwa
marehemu akiwa mahabusu aligonga kichwa chake kwa nguvu ukutani, hali
iliyosababisha wenzake kupiga kelele za kuomba msaada na kwamba baada ya
askari kufika na kukuta hali ilivyo, walimkimbiza Hospitali ya Taifa
Muhimbili kwa matibabu ambako alifariki dunia.
Marehemu Liberatus Damiani Temu enzi za uhai wake.
“Watu wanasemasema tu kwamba Liberatus aliuawa na askari, si kweli.
Kwa nini tumuue? Kwa kosa lipi? Sisi tulimshikilia kwa sababu hali ya
majeruhi aliyemgonga ilikuwa mbaya, hivyo kumweka mahabusu marehemu
ilikuwa kwa ajili ya usalama wake pia.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akifafanua jambo.
“Wengi wanaamini kila anayewekwa mahabusu ni mhalifu wa kiwango cha
kuteswa na polisi, si kweli. Wengine wanakaa hapa ili kuwalinda. Wewe
ukiua unadhani ndugu wa marehemu watakuacha?” alisema askari mmoja wa
kituo hicho bila kutaja jina lake kwa kuwa si msemaji mkuu.
Alisema kuwa mahabusu waliokuwa na marehemu ni mashahidi wakubwa kwamba jamaa alijigonga kichwa ukutani lakini kabla ya kufanya hivyo, alikuwa akisemasema maneno mengi kama aliyechanganyikiwa.
Hata hivyo, marehemu amezikwa akiacha maswali kibao, watu wanajiuliza je, kilichosemwa na polisi ndiyo ukweli au la! Kufuatia utata wa kifo hicho, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ameunda tume kufuatilia sakata hilo.
Alisema kuwa mahabusu waliokuwa na marehemu ni mashahidi wakubwa kwamba jamaa alijigonga kichwa ukutani lakini kabla ya kufanya hivyo, alikuwa akisemasema maneno mengi kama aliyechanganyikiwa.
Hata hivyo, marehemu amezikwa akiacha maswali kibao, watu wanajiuliza je, kilichosemwa na polisi ndiyo ukweli au la! Kufuatia utata wa kifo hicho, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ameunda tume kufuatilia sakata hilo.
0 comments:
Post a Comment