Na John Gagarini, Kibaha
MKAZI
wa Kijiji cha Bupu kata ya Bupu Tarafa ya Mkamba wilaya ya Mkuranga
mkoani Pwani Forodesi Ntabegera (30) ameuwawa kwa kubakwa kisha
kunyongwa na watu wasiojulikana kisha mwili wake kutupwa kichakani.
Kwa
mujibu wa taarifa ziliotolewa na kaimu kamanda wa polisi mkoani Pwani
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo Mrakibu Msaidizi wa Polisi (SSP)
Athuman Mwambalaswa Marehemu kuwa marehemu alinyongwa na watu hao kwa
kutumia kitenge chake alichokuwa amekivaa.
Kamanda
Mwambalaswa alisema kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 9 mwaka huu
majira ya saa 8:00 mchana baada ya wakazi wa kijiji hicho kufanya msako
wa kumtafuta marehemu ambaye alipotea Septemba 8.
“Baada
ya msako huo kufanyika mwili wa marehemu ulikutwa kwenye kichaka umbali
wa mita 30 kutoka barabarani ambapo mwili wake ulimwagiwa unga sehemu
za kichwani na mgongoni,” alisema Kamanda Mwambalaswa.
Alisema
watu hao walitumia mfuko wa salfeti aliokuwa amebebea unga aliotoka
kuusaga mashine, kumvisha miguuni kisha mwili wake waliulaza kifudifudi.
Aidha
alisema kuwa taarifa za kupotea marehemu zilitolewa na kituo cha polisi
Kimazinchana na mwenyekiti wa Kijiji cha Bupu Kasimu Kambangwa
walioongozana na watoto wa marehemu ambao walidai mama yao alitoweka
baada ya kuaga kuwa anakwenda kusaga na hakuonekana tena hadi mwili wake
ulipokutwa kwenye eneo hilo.
0 comments:
Post a Comment