Jeshi la
Nigeria linasema kuwa limewaua zaidi ya wanamgambo 100 wa kundi la Boko
Haram kufuatia shambulizi la wapiganaji hao siku ya ijumaa kazkazini
mashariki mwa jimbo la Borno.
Vikosi vya serikali vimeripotiwa
kuyakamata magari na risasi wakati vilipokuwa vikiimarisha usalama
katika mji wa Konduga,yapata kilomita 35 kutoka mji mkuu wa jimbo hilo,
Maiduguri.Wapiganaji wa Boko Haram wameiteka miji kadhaa na vijiji katika majuma ya hivi karibuni wakikaribia kuelekea Maiduguri.
0 comments:
Post a Comment