pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Hivi ndivyo Sitti Mtemvu alivyotwaa taji la Redd’s Miss Tanzania 2014

Sitti Mtemvu atwaa taji la Redd’s Miss Tanzania 2014 
MREMBO Sitti Abbas Mtemvu kutoka Temeke, juzi usiku alitwaa taji la Redd’s Miss Tanzania 2014, baada ya kuibuka kidedea katika fainali za shindano hilo lililofanyika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Sitti, mtoto wa Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu alitangazwa kuibuka kidedea katika shindano hilo na Mkurugenzi wa Lino Investment Agency, waratibu wa shindano hilo, Hashim Lundenga na kuwabwaga wengine 29.
Kwa ushindi huo, binti huyo wa Mtemvu, amerithi mikoba ya Happiness Watimanywa, mshindi wa taji hilo wa mwaka jana.
Katika shindano hilo lililoanza majira ya saa 4:00 usiku, lilishuhudia warembo wote 30 kutoa shoo kali ya ufunguzi kabla ya kupita jukwaani wakiwa na mavazi ya kubuni, ufukweni na vazi la usiku kabla ya kutangazwa kwa 15 bora, huku Sitti akionekana kuwa na sapoti kubwa jukwaani.
Baada ya kutangazwa kwa 15 bora washiriki walioingia tano bora walitangazwa na kila mmoja kuulizwa swali lake huku huku Sitti akitumia lugha ya Kifaransa na Kiingereza kujibu swali aliloulizwa.
Nafasi ya pili katika shindano hilo lililopambwa na burudani kutoka kwa Vanessa Mdee na Ommy Dimpoz, ilikwenda kwa Lillian Kamazima, huku mrembo wa Ilala Jihhan Dimachk akishika nafasi ya tatu, Dorice Mollel na Nasreem Abdul walishika nafasi ya nne na tano.

0 comments:

Post a Comment