Ripoti ya Environmental Investigation Agency (EIA) imedai kwamba Raisi wa china Xi Jinping na wafuasi wake waliozuru nchini Tanzania ndege waliokuja nayo ilitumika kibeba Meno ya tembo waliporudi nyumbani kwao China,
Inadaiwa kuwa wanunuzi, raia wa Uchina walinunua maelfu ya kilo za
pembe za ndovu nchini Tanzania na kuzitorosha kutoka nchini humo katika
ndege ya kibinafsi ya raia wa Uchina Xi Jinping,wakati alipozuru bara
Afrika.
Kulingana na shirika la ujasusi la mazingira lililo na makao yake mjini London.Pembe hizo zilinunuliwa wiki moja tu kabla ya ziara ya rais huyo wa Uchina nchini tanzania mwaka ulioipita ambapo zilifichwa katika mifuko ya wanadiplomasia ili kutokamatwa.
Shirika hilo pia linadai kwamba wajumbe waliokuwa wakiandamana na Rais Xi walinunua viwango vikubwa vya pembe hizo.
Uuzaji wa Pembe za ndovu ulipigwa marufuku mwaka 1989 ili kuwazuia wawindaji haramu kuwaua ndovu.
Dokezo: Tanzania ilikuwa na jumla ya Tembo wapatao 142,000 mwaka 2005 na hivi leo wamebaki Takribani Tembo 55,000 hii inatokana na uwezo mdogo wa Watanzania kulinda Rasilimali zao
0 comments:
Post a Comment