Mgeni
Rasmi Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani
(wa tatu kushoto) pamoja na wageni wengine waliohudhuria Sherehe hizo. Kutoka
kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Uchumi, Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Felix
Samilani, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Raphael M. Muhuga, Mkuu
wa Wilaya ya Tarime Mhe. John Henjewele, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara, na Mkuu wa Kiteule cha Bulamba Meja David Msakulo.
Mgeni
Rasmi Waziri wa Maendeleao ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani
(MB) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa Ufugaji wa Samaki ndani ya
Ziwa Viktoria Kiteule cha Bulamba kwa kutumia teknolojia mpya ya vizimba (Cages). Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya
Tarime Mhe.John Henjewele, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara. Kulia ni Mkuu wa Jeshi
la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael M. Muhuga.
Waziri
wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani akipandikiza
vifaranga vya samaki ndani ya Ziwa Victoria, mradi unaotekelezwa na Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT) Wilaya ya Bunda, Kiteule cha Bulamba kwa kutumia teknolojia
mpya hapa nchini ya kuzalisha samaki kwenye vizimba.
Picha
ya vizimba ambavyo ufugaji wa samaki umeanza mara baada ya Waziri wa Maendeleo
ya Mifugo na Uvuvi kuzindua mradi huo na kupandikiza vifaranga vya samaki.
Mradi unatekeleza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilaya ya Bunda, Kiteule cha
Bulamba kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Economic Social Research Foundation (ESRF), Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Ufugaji wa samaki
kwa kutumia teknolojia ya vizimba ndani ya Ziwa Victoria, umekuwa ukitekelezwa
pia na wenzetu wa Kenya na Uganda ambao wamepiga hatua kubwa .
Mkuu
wa Kiteule cha Bulamba, Meja David Msakulo
akitoa neno kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja (JKT)
Jenerali Raphael M. Muhuga ili azungumze na wananchi wa kijiji cha Bulamba.
Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Mratibu Mwandamizi wa Mradi Bw. Nehemia
Murusuri (wa kwanza kulia) pamoja na Mwakilishi wa Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Mratibu wa Mradi wa Kuondoa Umaskini, Kukuza Uchumi na Utunzaji
Endelevu wa Mazingira, Bw. Telesphory Kamugisha (wa pili kulia). Wengine ni
baadhi ya wageni waliohudhuria sherehe hizo.
Mkuu
wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael M. Muhuga akiongea na
wananchi wa Kijiji cha Bulamba wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Ufugaji wa samaki
katika Ziwa Victoria kwa kutumia teknolojia ya vizimba (Cages) ambayo ni teknolojia mpya ndani ya nchi yetu.
Waziri
wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani akitoa hotuba
kwa wananchi wa kijiji cha Bulamba (hawapo pichani) mara baada ya kuzindua Mradi wa Ufugaji wa
Samaki ndani ya Ziwa Viktoria. Aliwasisitiza wananchi kujiunga katika vikundi
ili kujijengea uwezo wa kuanza kutumia teknolojia ya kisasa ya kuzalisha samaki
kwa kutumia vizimba (Cages) katika
ziwa Victoria.
Waziri
wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (mwenye
Kaundasuti nyeusi) akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma ya asili mara baada
ya uzinduzi wa mradi huo.
Picha na: Thomas Nyindo, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
0 comments:
Post a Comment