Marekani imesitisha safari za ndege kuelekea kwenye uwanja mkubwa wa ndege wa kimataifa wa Ben Gurion ulioko Israili.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya kombora la
wanamgambo wa Hamas kuanguka takriban kilomita moja u nusu kutoka
kwenye uwanja huo.Punde baada ya onyo hilo la (FAA) Mashirika kadha ya ndege ya bara uropa pia yalichukua hatua sawa na hiyo.
Mashirika hayo Lufthansa, KLM, na Air France pia yamesitisha safari kuelekea Tel Aviv.
Lufthansa - ambayo ni muungano wa mashirika ya ndege ya Uswissi, Ujerumani na shirika la ndege la Austria imetangaza kusitisha safari kuelekea Israili kwa siku mbili.
Mashirika ya ndege ya KLM na Air France yameahirisha safari zilizokuwa zimeratibiwa kuanza jumanne.
Delta ambayo ilikuwa imeratibu safari ya ndege kutua Tel Aviv ililazimika kutua Ufaransa baada ya polisi nchini Israili kudhibitisha kuwa kombora hilo lilitua kilomita moja nukta 6 kutoka kwenye uwanja huo wa Ben Gurion.
Kusitishwa kwa safari hizo za ndege zinawadia wakati Israili ikiendelea na vita dhidi ya Wapalestina huko Gaza.
Cha mno kwa mashirika ya ndege ni taharuki ya usalama wa ndege za abiria zinazopitia katika anga za mataifa yaliyo na vita haswa baada ya tukio la hivi punde ambapo ndege ya Malaysia MH17 kudenguliwa mashariki mwa Ukraine.
0 comments:
Post a Comment