Wapiganaji wa kundi la Islamic State wafungua kambi za mafunzo Libya
Wapiganaji
wa kundi la Islamic State wameanzisha kambi za mafunzo mashariki mwa
Libya, amesema mkuu wa kamandi ya Marekani ya masuala ya Afrika.
Jenerali David Rodriguez
amesema kuna mamia ya wapiganaji wa IS wanaopata mafunzo ya kijeshi
kwenye kambi zake nchini Libya. Amesema kambi hizo zipo katika hatua za
mwanoz kabisa, lakini Marekani imekuwa ikiyafuatilia kwa karibu kuona
zinavyoendelezwa.
Libya imekuwa katika mgogoro tangu kuangushwa
kwa utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011, ambapo makabila mbalimbali,
wanamgambo na makundi ya kisiasa, wote wakipigania madaraka.
Makundi
mbalimbali ya Kiislam yanawania madaraka mashariki mwa Libya, huku
baadhi yakitangaza kuwa na ushirikiano la kundi la Islamic State, IS.
Akizungumza mjini Washington Jumatano, Jenerali Rodriguez bado haijafahamika ukaribu uliopo kati ya watu wanaopata mafunzo hayo na kundi la IS.
"Kikubwa
ni watu wanaokuja kupata mafunzo na msaada wa vifaa kwa ajili ya kambi
za mafunzo kwa sasa," amesema. "kwa sasa mafunzo hayo bado ni ya hatua
ya chini sana na tunafuatilia kuona namna hali inavyokwenda."
Waandishi wa habari wanasema
katika kipindi cha mapinduzi yaliyomwondoa madarakani Gaddafi,
wapiganaji wengi waasi waliondoka nchini humo kwenda kujiunga na vikundi
vya wapiganaji nchini Syria na baadhi yao wanaaminika kuwa wamerejea
nyumbani(Libya).
Serikali iliyochaguliwa imepoteza miji mikuu mitatu ya Libya huku kukiwa na mgogoro wa kisiasa.
Benghazi,
mji wa pili kwa ukubwa nchini Libya, uko mikononi mwa wapiganaji wa
Kiislam, na bunge linalotambuliwa kimataifa kwa sasa linaendesha vikao
vyake katika mji ulioko pwani ya Tobruk mashariki mwa nchi hiyo.
Marekani
imekuwa ikiongoza washirika wa kimataifa kufanya mashambulio ya anga
dhidi ya IS nchini Iraq na Syria katika miezi ya karibuni.
0 comments:
Post a Comment