Tukio hilo la aina yake lilitokea Novemba 22, mwaka huu saa 6 usiku
katika wodi ya majeruhi baada ya mtuhumiwa huyo kuzua tafrani kwa kutaka
kupiga wenzake, hali iliyosababisha wagonjwa mbalimbali kutimua mbio na
kujificha kuokoa maisha yao na kumuacha marehemu ambaye alikuwa
hajiwezi akiwa amelala kitandani.
Kwa
mujibu wa shuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa, Hashimu ambaye bado
amelazwa katika wodi hiyo akiwa amefungwa pingu mkononi, chini ya ulinzi
wa polisi, alieleza kuwa mnamo muda huo mtuhumiwa alitenda kosa hilo
baada ya kumaliza kuswali.
“Kabla ya kuanza swala mtuhumiwa huyo alimuomba kijana aliyekuwa akimuuguza ampeleke kujisaidia,” alisema shuhuda huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe.
Aliongeza
kuwa baada ya kurejea alipiga magoti na kuanza kuswali chini ya
kitanda alichokuwa amelazwa na baadaye alipomaliza aliwaamuru wagonjwa
wenzake wazime taa.
“Baada ya taa hizo za wodini kuzimwa mtuhumiwa alisikika
akisema
kwa sauti kubwa kuwa leo anataka kuua mtu huku akivurugavuruga vitu
kwenye vitanda vya wagonjwa kikiwemo cha kwake na kupiga kelele kwa
sauti kubwa, hali iliyowafanya wagonjwa wengine kutimua mbio. Hata
hivyo, wakati vurugu hizo zikiendelea muuguzi wa zamu alitoa taarifa kwa
kupiga simu kituo cha polisi mjini kati.
Wakati
askari polisi wakisubiriwa mtuhumiwa aliendelea na vurugu na kuchukua
chuma cha kutundikia drip na kuivunja kisha kwenda kumpiga kichwani
marehemu aliyekuwa amelala pekee kwenye wodi hiyo akiuguza mguu wake wa
kulia na alifariki dunia papo hapo.
0 comments:
Post a Comment