Na
Saidi Mkabakuli, Kigoma
Serikali imeazimia kuanza
kufanya utanuzi wa Kiwanja cha Ndege Kigoma ili kuweza kukidhi mahitaji
yanaongeza siku baada ya siku ya kiwanja hicho.
Azma imetolewa na Kiongozi wa
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango,
Bibi Florence Mwanri wakati walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miundombinu
katika Uwanja wa Ndege wa Kigoma.
Bibi
Mwanri alisema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini ipo kwenye
mkakati wa kuuendeleza uwanja huo ili uwe wa kiwango kizuri kwa kuhudumia
watumiaji wa wa kiwanja hicho.
“Kama munavyokumbuka
Serikali katika mwaka ujao wa fedha imepanga kuendeleza na kuboresha
miundombinu ya usafiri wa anga ili kuongeza ufanisi; na kuendelea na kazi ya
ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege katika maeneo ya kimkakati ikiwamo
Kiwanja cha Ndege cha Kigoma,” alisema.
Kwa mujibu wa Bibi
Mwanri, uendelezaji wa Kiwanja hicho utajumuisha ujenzi wa jengo la abiria
pamoja na miundombinu yake (maegesho ya ndege, maegesho ya magari na barabara
ya kuingia na kutoka) na kurefusha barabara ya kuruka na kutua ndege.
Akiwasilisha taarifa ya
maendeleo ya uwanja huo, Meneja Mradi wa Utanuzi wa Kiwanja cha Kigoma,
Mhandisi Neema Mwasha alisema kuwa mpaka sasa Mamlaka
ya Usimamizi wa Viwanja vya Ndege nchini imekamilisha taratibu za kumpata mkandarasi kwa
ajili ya ujenzi wa uzio wa usalama na eneo la maegesho ya ndege.
“Kwa sasa tunaendelea na
kazi ya utayarishaji wa makabrasha ya zabuni kwa ajili ya kazi za ujenzi wa
barabara ya kuingia kiwanjani, maegesho ya magari, na usanifu wa kina kwa ajili
ya upanuzi wa maegesho ya ndege pamoja na usimikaji wa taa na mitambo ya
kuongozea ndege,” alisema.
Mhandisi Neema aliongeza
kuwa wapo kwenye mchakato wa kumpata Mhandisi Mshauri wa kufanya usanifu wa
jengo la abiria uwanjani hapo.
Naye Kaimu Meneja wa
Kiwanja cha Ndege Kigoma, Bw. Joseph Nyahende alisema kuwa katika kuhakikisha
kazi hiyo inafanyika kwa wakati, Mamlaka
ya Usimamizi wa Viwanja vya Ndege nchini kwa kushirikiana na Mkoa wa Kigoma
vimeainisha na kufanyia tathmini eneo litakalotumika kwa ajili ya kazi hiyo.
Kaimu Meneja wa Kiwanja
cha Ndege Kigoma, Bw. Joseph Nyahende (Wapili kushoto) akitoa maelezo kuhusu Kiwanja
cha Ndege Kigoma kwa Kiongozi wa
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango,
Bibi Florence Mwanri (Kulia). Wanaosikiliza ni Meneja Mradi wa Utanuzi wa Kiwanja cha Kigoma,
Mhandisi Neema Mwasha (Kushoto) na Bw. Julius Edward (Wapili kulia).
Meneja Mradi wa Utanuzi
wa Kiwanja cha Ndege Kigoma, Mhandisi Neema Mwasha (Kushoto) akifafanua jambo
kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya
Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mara walipofika kujionea
shughuli za maendeleo kiwanjani hapo.
Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa
Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri
(Wapili kulia) akisisitiza jambo wakati akiongea na Kaimu Meneja wa Kiwanja cha Ndege
Kigoma, Bw. Joseph Nyahende (Wapili kushoto) na Meneja Mradi wa Utanuzi wa
Kiwanja cha Kigoma, Mhandisi Neema Mwasha (Kushoto).
Sehemu ya Kiwanja cha Ndege Kigoma ikiwa imekamilika kwa kiwango cha lami.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya
Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakionesha eneo lililoainishwa na kufanyiwa tathmini kwa ajili ya kazi ya
utanuzi wa Kiwanja hicho.
Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na
Ufuatiliaji (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bw. Omary Abdallah (Kulia)
akiuliza jambo wakati wakioneshwa eneo lililoainishwa
na kufanyiwa tathmini kwa ajili ya kazi ya utanuzi wa Kiwanja hicho.
Kaimu Meneja wa Kiwanja
cha Ndege Kigoma, Bw. Joseph Nyahende (Aliyenyanyua mikono) akitoa maelezo juu
ya sehemu zitakazoendelezwa kwa Timu
ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Meneja Mradi wa Utanuzi
wa Kiwanja cha Ndege Kigoma, Mhandisi Neema Mwasha (Wapili kulia) akionesha
eneo likaloboreshwa katika Mradi wa Utanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kigoma.
Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya
Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akiangalia tabaka za udongo
uliotumika katika kujengea Kiwanja cha Ndege Kigoma. Anayemuonesha ni Kaimu
Meneja wa Kiwanja cha Ndege Kigoma, Bw. Joseph Nyahende (Kulia).
PICHA ZOTE NA SAIDI MKABAKULI
0 comments:
Post a Comment