Huku viongozi wa al-Shabaab wakiuawa katika mashambulizi ya anga
yaliyolengwa na wapiganaji wake kuasi kwa idadi kubwa, serikali ya
Somalia na washirika wake wana fursa ya kutumia faida ya hali dhaifu ya
kundi hilo, wachambuzi wanasema.
"Hasara ambayo al-Shabaab imekuwa ikipata kwa mfululizo katika miaka
miwili iliyopita inaonekana kuwa ni tishio kwa uwepo wa kundi hilo,"
alisema Abdirahim Isse Addow, mkurugenzi wa Redio Mogadishu
inayoendeshwa na serikali na msemaji wa zamani wa Umoja wa Mahakama za
Kiislamu, umoja ambalo al-Shabaab ilijitenga nalo.
"Ishara za kutengana kwa al-Shabaab ni dhahiri sana," Addow aliiambia
Sabahi. "Hakuna kikundi kinaweza kuendelea kuwepo wakati kinapoteza
uungwji mkono na jamii ambayo ipo ndani yake."
Kutokana na matokeo ya mashambulizi ya Seriklai ya Somalia na Kikosi
cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika Somalia, (AMISOM), al-Shabaab
imepoteza mapato ambayo ilikuwa ikipata kutoka miji muhimu kama vile Barawe, Kismayu, Bulo Burde na El Bur, alisema.
Aidha, alisema, migogoro ya ndani ya al-Shabaab,
ambayo imeikumba kikundi katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita,
imekuwa na athari za kudumu katika kuvunja uongozi wa kikundi hicho.
Migawanyiko ndani ya kikundi hicho ilikuwa mikubwa sana ambayo hatimaye ilipelekea kiongozi wa zamani wa al-Shabaab Ahmed Abdi Godane kuandaa mauaji ya makamanda wengi wa zamani, ikiwa ni pamoja na mwanzilishi mwenza wa al-Shabaab Ibrahim Meeaad al-Afghani, mpiganaji jihadi mzaliwa wa Marekani Abu Mansour al-Amriki na Maalim Burhan, Addow alisema.
"Baada ya hapo, watu wengine wengi ambao waloikuwa sehemu ya kikundi hicho walikimbia, wakiwemo Mukhtar Robow, Hassan Dahir [Aweys] na Zakariya [Ismail Ahmed Hersi], ambaye hatimaye alijisalimisha kwa serikali," alisema.
Kikundi hicho kamwe hakikurejea kuotka hali ya kuvunjika katika uongozi wake, ambao sasa umekuwa ukimalizwa kwa mashambulizi ya anga yanayowaua viongozi waliobakia, Addow alisema.
Katika mfano wa karibuni zaidi wa shambulio la anga lililofanikiwa dhidi ya uongozi wa al-Shabaab, mkuu wa upelelezi wa kikundi hicho Abdinasir Hassan Barakobe,
ambaye majina yake mengine yalikuwa ni pamoja na Abdishakur na Tahlil,
aliuawa tarehe 29 Disemba karibu na Saakow, kwenye Mkoa wa Jubba ya Kati
nchini Somalia.
Kifo chake kilikuja siku mbili baada ya kujisalimisha kwa mkuu wa upelelezi wa al-Shabaab Hersi kwa mamlaka za Somalia.
Kabla ya kuuawa, mengi yalikuwa hayajulikani kuhusu Barakobe, ambaye
alikuwa katika umri wa miaka 30 na alizaliwa katika familia maarufu huko
wilaya ya Bondhere mjini Mogadishu. Alikuwa mmoja wa maafisa wa Umoja
wa Mahakama za Kiislam na baadaye alijiunga al-Shabaab mwaka 2007
Barakobe alikuwa akiaminika kuwa alikuwa karibu sana na Godane na
baada ya kifo chake iliibuka kuwa yeye ndiye aliyekuwa na dhamana wa kitengo cha upelelezi cha Amniyat
Fursa ya kuiangamiza al-Shabaab
"Serikali ya Somalia ina fursa kubwa ya kuliangamiza kundi hili kwa
msaada wa washirika wake," alisema Abdirisaq Mohamed Qeylow, ambaye
alikuwa msemaji wa Muungano wa Mahakama za Kiislamu kabla ya kujiunga na
serikali ya Somalia na kuwa msemaji wa Wizara ya Habari chini ya Rais
Sheikh Sharif Sheikh Ahmed wa Serikali ya Mpito ya Shirikisho.
"Kipindi cha msamaha
kinapaswa kuongezwa na fursa zilizotolewa kwa watu ambao hawajafanya
makosa makubwa, kama vile vijana, lazima ziongezwe kama vile elimu, kazi
na kuwahakikishia usalama wao kama njia ya kuwavutia vijana ambao bado
wamo kwenye kundi hilo," aliiambia Sabahi.
Hatima ya wanachama wa al-Shabaab ni katika ya vigawe vitatu, kwa mujibu wa Qeylow.
"Kwanza ni viongozi wakuu wa kundi hilo, ambao baadhi yao wamefanya
makosa makubwa dhidi ya watu wa Somalia," alisema. "Haitawezekana kwao
kujificha ndani ya jamii na serikali ya Somalia haiwezi kufanya maamuzi
juu yao peke yake ikiwa watajisalimisha kwa sababu wamefanya makosa
makubwa dhidi ya dunia. Hivyo, watajaribu kupigana hadi wauawe."
"Kuna kundi la pili. Hawa ni watu ambao hawafahamiki sana na watu,
lakini wana nguvu kwenye kundi hilo. Hao ni watu walio na fursa ya
kujisalimisha na kujitenga mbali na shughuli walizokuwa wakijihusisha
nazo wakiwa sehemu ya al-Shabaab," alisema. "Kundi la tatu ni wanachama
vijana wa al-Shabaab ambao wanabeba silaha. Hao hujisalimisha kila siku na na kurekebishwa kitabia."
"Kundi hili halitaweza kuendelea kubakia kama mambo yanakwenda kama hivi," Qeylow aliongeza.
Ugumu wa al-Shabaab katika kuwabakisha wapiganaji wake wa kigeni na kuwavutia wapya pia unaonesha matatizo ya kundi hilo.
"Katika siku za karibuni kumekuwa hakuna habari juu ya wapiganaji wa
kigeni wanaopigana upande wa al-Shabaab. Nadhani wengi wao wameondoka
nchini na wamejiunga na mapigano yanayoendelea kwenye nchi za Kiarabu
kama Libya, Yemen na Syria," alisema Qeylow. "Jambo hilo limedhoofisha
nguvu za al-Shabaab, ambayo mwanzoni ilikuwa inaungwa mkono kiitikadi na
kifedha na al-Qaida."
"Inawezekana kwamba baada ya kuuawa kwa Fazul Abdullah Mohammed, ambaye alikuwa mkuu wa al-Qaida kwenye eneo la Afrika Mashariki na aliyekufa kwenye mtego wa Godane, na barua ya malalamiko iliyoandikwa na Ibrahim al-Afghani, ambaye pia aliuawa na Godane, kulishusha uungaji mkono wa al-Qaida na makundi mengine (kwa al-Shabaab)," alisema.
Kupambana na itikadi ya al-Shabaab
Wimbi la kushindwa lililoikumba al-Shabaab katika siku za karibuni
limeufanya uongozi wake kusambaratika na kundi hilo kudhoofika, alisema
mchambuzi wa masuala ya kisiasa Hassan Sheikh Ali, lakini itikadi kali
ambalo kundi hilo linaisambaza itaendelea nchini Somalia kwa miaka mingi
ijayo.
"Al-Shabaab imekuwa ikienda chini kwa miaka mitatu iliyopita, lakini
mauaji ya hivi karibuni ya viongozi wao wa juu yatatumika kwa kuharibu
[kudumu] uwezo wa kijeshi wa kundi, nguvu na ari hivi karibuni," Ali
aliiambia Sabahi. "Lakini kama itikadi, al-Shabaab itakuwa hapa kwa muda
mrefu na itabi8di ipigwe vita kwa itikadi nyingine."
"Al-Shabaab inaumia pia kwa sababu wapiganaji wa kigeni waliokuwa
wakija hapa kwa ajili ya jihadi sasa wanakwenda Syria na Iraq," alisema.
"Kwa hivyo, serikali ya shirikisho ya Somalia, serikali za mikoa na
majimbo, na jamii ya kimataifa lazima zichukue fursa kwa hali ya
kudhoofika ya al-Shabaab iliyonayo sasa."
"Ili kufanya hivyo, serikali lazima iepuke migogoro ya kisiasa ambayo inaudhoofisha uwezo wake wa kufanya kazi," alisema.
Kundi kama al-Shabaab linaweza tu kudumu ikiwa lina uongozi imara,
alisema Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana wa Somalia, Mukhtar Haji
Kastaro. "Lakini [msingi wa] al-Shabaab umeharibiwa. Katika miezi
michache ya hivi karibuni, viongozi wake wengi wakuu wameuawa na
serikali isipoteze fursa hii," aliiambia Sabahi.
"Baadhi ya hatua ambazo serikali na AMISOM wanapaswa kuzichukuwa ni
pamoja na kuchukuwa udhibiti wa haraka wa wilaya zilizo chini ya
al-Shabaab ili kutowapa fursa ya kujikusanya tena, kujiingiza kwenye
mazungumzo na viongozi wa al-Shabaab wenye msimamo wa wastani na
kuendelea kuwaandama [kwa kuwauwa] wale wachache wenye siasa kali
waliobakia kwenye kundi hilo."
"Hilo likifanyika, al-Shabaab inaweza kuharibiwa moja kwa moja ndani
ya kipindi cha miezi 12 ijayo kwani inapumua upumzi wake wa mwisho,"
alisema.
0 comments:
Post a Comment