Kiongozi wa kanisa katoliki papa
francis anaongoza misa ambayo imehudhuriwa na watu wengi katika bustani
ya Rizak kwenye mji mkuu wa Ufilipino Manila akiwa kwenye siku ya mwisho
ya ziara yake barani Asia.
Waandalizi wanasema kuwa watu milioni kadhaa wamehudhuria misa hiyo licha ya kuwepo kwa mvua.
Misa hiyo inatajwa kuwa iliyohudhuriwa na watu wengi zaidi tangu papa John Paul wa pili azuru eno hilo mwaka 1995.
Picha
za televisheni zilionyesha watu wengi katika bustani ya Razal wakipunga
mikono na kushangilia wakati papa alipokuwa akipita akiwa ndani ya gari
lake.
0 comments:
Post a Comment