Mmoja kati ya majambazi waliokamatwa akiwa amelala chini baada ya kujeruhiwa na polisi.
Tukio la ujambazi limesababisha watu
wawili kujeruhiwa na watatu kupoteza fahamu kutokana na vishindo vya
risasi na mabomu wakati majambazi hayo yalipotaka kutoroka. majambazi
hayo yalikuwa na gari aina ya Toyota Noah yalikimbizana na polisi na
walipofika katika kituo cha zamani cha daladala walipotea njia kabla ya
gari yao haijakwama katika ukuta wa Shule ya Msingi Darajani
Askari polisi akiwa sehemu ya tukio(PICHA/LM)
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alisema majambazi
hayo yalikuwa yamegawanyika makundi mawili huku wengine yakifanikiwa
kukimbilia katika eneo la Fumba lililopo nje ya mji
Jambazi akiwa kwenye gari ya polisi baada ya kukamatwa.(PICHA/LM)
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alisema majambazi
hayo yalikuwa yamegawanyika makundi mawili huku wengine yakifanikiwa
kukimbilia katika eneo la Fumba lililopo nje ya mji.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam,
Majambazi hao wamekamatwa Darajani
Zanzibar jana baada ya kufyatuliana risasi na polisi wakati wakijaribu
kukimbia. Katika tukio hilo wananchi kadhaa walijeruhiwa kwa kugongwa na
gari katika harakati za majambazi hayo kukimbia. Polisi imewatia
mbaroni majambazi watatu baada ya wananchi kutoa ushirikiano.
0 comments:
Post a Comment