Mwenyekiti
wa Tume ya Uchaguzi nchini Zambia, Bi Irene Mambilima jana alisitisha
zoezi la kutoa matokeo ya uchaguzi mkuu akisema tume imefanya hivyo ili
vituo vingine 51 navyo vikamilishe utaratibu wa kupiga kura leo.
Hata
hivyo Bi Mambilima alikabiliwa na watu wenye ghadhabu wakitaka Tume ya
Uchaguzi iendelee kutoa matokeo ya chama kilichoshinda maana tume hiyo
ilikuwa tayari imeshatangaza matokeo ya majimbo 14.Hata hivyo mwenyekiti huyo wa Tume ya Uchaguzi ya Zambia amesisitiza kuwa uamuzi huo una manufaa kwa wadau wote, ili kutenda haki.
"Tunaendesha uchaguzi katika nchi hii, tunafanya maamuzi na katika kufanya maamuzi hayo hatulazimiki kupokea maagizo kutoka kwa mtu yeyote. Tumefanya maamuzi. Watu wengine wanasema tufikirie tufikirie. Mnaendelea kurudia mambo hayo hayo kila wakati. Hii si jamii ya malumbano. Tumewaambia maamuzi yetu ni nini, unaweza kukubali au kukataa. Tunaendesha uchaguzi katika nchi hii, SAWA? Kwa kuwa hamkubali hakutakuwa na rais,"anasema Bi Mambilima.
Uchaguzi wa rais nchini Zambia unafanyika kufuatia kifo cha rais Michael Sata, aliyefariki dunia mwaka jana.
0 comments:
Post a Comment