Mwenyekiti wa Kitongoji
cha Songambele, Kata ya Ilela Tarafa Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoa wa
Katavi, Richard Madirisha (31), ameuawa kikatili kwa kuchinjwa shingo
na kutenganishwa na kiwiliwili na kisha kunyofolewa viungo vya mikono
na miguu na sehemu za siri na kichwa chake na viungo hivyo kupikwa
ndani ya safuria kama mboga.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari mauaji hayo ya kikatili na
kutisha yalitokea jana saa 5.30 usiku nyumbani kwa marehemu.
Kidavashari alisema, siku hiyo
ya tukio marehemu alikuwa amelala nyumbani kwake akiwa na mkewe
Meklina Mussa na ghafla walitokea watu watano ambao hawafahamiki na
kuvunja mlango na kuingia ndani ya nyumba.
Alisema watu hao waliodaiwa kuwa
na mapanga waliingia chumbani kwa marehemu na kumlazisha mkewe
ajifiche kwa kujifunika na shuka usoni.
Alisema baada ya mkewe
kujifunika walianza kumchinja marehemu kwa kutumia panga huku mkewe
akiwa anasikia jinsi marehemu akilia kwa uchungu.
Kidavashari alisema baada ya
kumchinja walichukua kichwa na kukiweka kwenye safuria na maji na
kukipika kwenye moto uliokuwa unawake nje ya nyumba ya marehemu.
Alisema kisha walirudi ndani na
kunyofoa sehemu za siri, mikono na miguu na kuziweka kwenye safuria
jingine kwenye moto na kutokomea kusikojulikana huku viungo hivyo
vikiendelea kuchemka ndani ya safuria hizo.
Kidavashari alisema mke wa
marehemu baada ya kuona watu hao wametokomea alitoka nje na kwenda kutoa
taarifa kwa majirani ambao walifika kwenye eneo hilo na kukuta viongo
hivyo vikiwa ninaendelea kuchemke kwenye safuria hizo huku kiwailiwili
chake kikiwa ndani ya chumba chake
Amesema uchunguzi wa awali
umebaini kuwa chanzo cha mauwaji kimetokana na visa vya marehemu na mtu
mmoja ambae walikuwa wakiishi nae Tabora ambae alikuwa akimtuhumu
marehemu kuwa amemnyanya mwanamke ambae walikuwa na mahusiano nae ya
kimapenzi ambae marehemu aliamua kuhama nae kijijini hapo na kuhamia
nae kijiji cha Songambele Wilaya Mlele
Kamanda Kidavashari alieleza
jeshi la polisi Mkoa wa Katavi limewakamata na linawashikilia watu
watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauwaji hayo ya kikatili
0 comments:
Post a Comment