Watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wamewavamia na kuwajeruhi askari mwenye no G369 PC
Mansour na Hv507 PC Mwalimu, wakiwa doria ya pikipiki ambao
walinyang’anywa silaha mbili aina ya SMG no 14301230 na 14303545 na watu
wasio julikana mkoani Tanga.
Taarifa
ya Jeshi hilo kwa vyombo vya habari imesema tukio hilo limetokea
Januari 26, 2015 majira ya saa 23:30hrs eneo la barabara 04 jijini humo.
Aidha,
imesema mmoja wa majeuhi askari mmoja no H 507 PC Mansour amejeruhiwa
vibaya maeneo mbalimbali ya mwili na amelazwa katika Hospitali ya Mkoa
Bombo.
Katika
uchunguzi wa awali Polisi wamefanikiwa kumtia hatiani mtuhumiwa mmoja,
Ayubu Haule, (27), fundi Radio Mkazi wa Corner Z Amboni Kiomoni ambaye
alikamatwa eneo la tukio akijaribu kutoroka na pikipiki na mara baada ya
kupekuliwa ndipo alipokutwa na mchoro wa ramani unaoonyesha matokeo ya
Barabara na kufunguliwa kesi yenye no TAN/IR/322/2015.
Mtuhumiwa
anaendelea kuhojiwa na Jeshi hilo huku timu ya Intel na makachero wa
Polisi ikiendelea kufanya doria pamoja na Section 2 za FFU.
Chanzo: JamiiForums
0 comments:
Post a Comment