Akiwa
na umri wa miaka 90 mwanamke wa Kenya ambaye anahudhuria masomo akiwa
na wajukuu zake wapatao sita inaaminika ndiye mwanafunzi mzee zaidi
anayesoma shule ya msingi duniani.
Akiwa ameketi dawati la mbele
kabisa darasani ,yuko darasa la tano na amevalia nguo za shule ,
Priscilla Gogo Sitienei anamsikiliza mwalimu anayefundisha kwa makini
hukua akiandika majina ya wanyama kwa kiingereza kwenye daftari lake.
Prissilla
alijiunga na shule hii ya Leaders Vision Preparatory School miaka
mitano iliyopita lakini pia aliwahi kuwahudumia wakaazi wa kijiji chake
cha Ndalat kilichoko kwenye bonde la ufa kama mkunga miaka sitini na
mitano iliyopita.
Darasani Priscilla anawasaidia wengine wafanye
vyema ambao wana umri kati ya miaka 10 hadi 14 na mar azote huwaambia
ujumbe wake hasa mabinti kuwa elimu ndiyo urithi wao.
Priscilla
anajulikana kama Gogo maana yake bibi katika lugha ya jamii ya
wakalenjini,anasefurahia masomo akiwa na umri wa miaka 90 katika umri
huo anajua kuandika na kusoma pia fursa aliyoikosa alipokuwa mdogo.
Lugha
ambayo Priscilla anajiona yuko huru kuitumia ni lugha mama kwake ki
Kalenjin kuliko kiingereza,pindi anapotakiwa kujieleza kwanini aliamua
kujiunga na shule katika umri wake.
Sababu kubwa ambayo amekuwa
akiitoa,ni ajue kusoma ili amudu kusoma bibilia,lakini pia kwa umri wake
anataka awahamasishe watoto kupata elimu,kwani anawaona watoto wengi
wakiwa hawako shuleni na watoto hao wana watoto.
Gogo apitapo
mitaani haoni shida kukabiliana na watoto ambao hawako shuleni katika
muda wa masomo na kuwauliza kwanini hawako shuleni.
Gogo anasema
watoto hao humjibu kwamba hawaendi shule kwakuwa umri wao ni mkubwa,name
huwaambia mimi ni mkubwa sana kwenu lakini niko shuleni hivyo nanyi
jiungeni na shule.
Kikubwa kinachomuumiza Gogo ni kuwaona watoto
wengi waliopoteza muelekeo,wengi wao hawana baba na wanazurura hovyo
mitaani,bila msaada wowote.kutokana na hali hiyo nataka kuwahamsisha
waende shuleni
0 comments:
Post a Comment