Wanafunzi
watatu ambao wanatuhumiwa kuwa vinara wa maandamano ya wanafunzi wa
programu maalumu ya walimu wa sayansi Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
wameachishwa masomo.
Wakati
mmoja wao akiwa amefukuzwa moja kwa moja, wawili wengine wana nafasi ya
kujieleza kuhusika kwao na maandamano hayo, yaliyochafua hali ya hewa
na kusababisha wanafunzi 84 kutiwa mbaroni.
Makamu
Mkuu wa chuo hicho, Profesa Idrisa Kikula akizungumza na Mpekuzi
alisema kwamba watu hao wameondolewa jana asubuhi cini ya ulinzi wa
polisi ili kurejesha utulivu katika chuo hicho.
Hata
hivyo, alisema hadi jana wanafunzi wote wakiwemo hao wa program maalumu
ya ualimu chuoni hapo walikuwa wanaendelea na masomo yao kama kawaida.
Aliwataja
walioondolewa shuleni hapo kuwa ni Kyambwene Msatu (Rais), Philip J
Mwakibinga (Waziri Mkuu) na Ismail Chande (Katibu Mkuu).
Alisema
Mwakibinga amefukuzwa moja kwa moja, kutokana na kiapo chake
alichokitia saini baada ya vurugu za mwisho katika chuo hicho, kwamba
hatajihusisha na uongozi na akirejea tena kutoa hamasa ya wanafunzi
kugoma na kuandamana, afukuzwe moja kwa moja.
Alisema
pamoja na hatua hizo zilizochukuliwa, wanaendelea na uchunguzi na
wahusika wengine, kwani wamefanya mambo kinyume na taratibu za chuo na
serikali.
Alisema
Chuo kiliwaeleza wanafunzi bayana kwamba kama wana kitu, wafuate
taratibu ili Chuo kiwasilishe malalamiko yao kwa mfadhili wao, ambao ni
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Hata
hivyo, alisema hawakufuata na baadaye kuanza kuwa na mikutano haramu
na kuamua kuandamana usiku huku wakiwashinikiza wenzao kwa kuwapiga kama
hawatashiriki.
Juzi
katika maandamano hayo, polisi walisema kwamba wamekamata wanafunzi 84
ambao walikuwa wakiandamana kutoka chuoni hapo kuelekea katika Ofisi za
viongozi wa Serikali zilizopo Dodoma mjini majira ya saa 11 alfajiri.
Profesa
Kikula alisema wakati maandamano hayo yanafanyika kwa bahati ilikuwa
siku ya baraza kamili la vyuo, ambalo limeridhia hatua zilizochukuliwa
dhidi ya wanafunzi hao watatu, zilizolenga kuwapisha wenzao kuendelea na
masomo.
0 comments:
Post a Comment