pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

EU yarefusha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Zimbabwe

EU yarefusha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Zimbabwe
Umoja wa Ulaya umetangaza kurefusha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Zimbabwe kwa mwaka mmoja zaidi.
Umoja huo pia umerefusha vikwazo vya usafiri dhidi ya Rais Robert Mugabe na mke wake Grace Mugabe. Taarifa ya EU imesema vikwazo hivyo vitaendelea hadi Februari 20 mwaka ujao wa 2016. Taarifa ya Umoja wa Ulaya pia imesema vikwazo vya usafiri dhidi ya Rais Mugabe vinaweza kusimamishwa kwa muda iwapo atahitajika kusafiri Ulaya kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika.
Umoja wa Ulaya uliiwekea Zimbabwe vikwazo vya kiuchumi mwaka 2002 kwa madai ya kutokea udanganyifu kwenye uchaguzi pamoja na kuweko kile kinachodaiwa kuwa ni ukiukaji wa haki za binadamu katika nchi hiyo.
Rais Mugabe amekuwa akiwakosoa viongozi wa Ulaya hususan Uingereza akisema lengo lao kuu ni kudumisha ukoloni mamboleo katika nchi za Afrika.

0 comments:

Post a Comment