
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya
Kiislamu ya Iran yaani bunge Ali Larijani amesema kuwa serikali ya Iran
na wananchi kamwe hawatalegeza kamba juu ya haki zao za kinyuklia.
Larijani ameyasema hayo huku Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiendeleza
mazungumzo yake na kundi la 5+1 ili kufikia makubaliano kamili kuhusu
miradi yake ya nyuklia. Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran
amesema kuwa madola yenye nguvu yanataka kuzuia maendeleo ya Iran katika
sayansi ya nyuklia kwa kuibua changamoto katika uga wa kimataifa. Hata
hivyo Iran haitaachia haki zake za nyuklia. Larijani amesisitiza kwamba
mashinikizo na vikwazo vya madola yenye nguvu havitakuwa na taathira kwa
miradi ya nyuklia ya nchi hii yenye malengo ya amani
0 comments:
Post a Comment