
Kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh, limewaua kwa
kuwachoma moto Wairaq 50 mjini Hīt kaskazini magharibi mwa mji wa
al-Ramadi nchini Iraq. Televisheni ya serikali ya al-Iraqiya
imethibitisha habari hiyo na kuongeza kwamba kundi hilo limetekeleza
jinai hiyo dhidi ya watu hao kufuatia fatwa iliyotolewa na masheikh wa
Kisalafi wa Kiwahabi kwa kutegemea maandishi ya vitabu vya Ibn Taymiya.
Ni vyema ifahamike kuwa tangu kundi hilo lilipotekeleza mauaji dhidi ya
Muadh al-Kasasbeh, rubani wa Jordan aliyeuawa kwa kuchomwa moto na
wanachama wa Daesh, kundi hilo la kitakfiri limeendeleza mlolongo wa
jinai hizo ambapo karibu kila siku watu kadhaa huuawa kwa njia hiyo. Kwa
mujibu wa habari, siku chache zilizopita, wanachama wa Kidaesh,
waliwaua watu wengine 45 katika viunga vya mji wa al-Baghdadi, magharibi
mwa Iraq. Awali Wizara ya Ulinzi ya Iraq, ilikuwa imetangaza kuwa jeshi
la nchi hiyo limewaangamiza wanachama 23 wa kitakfiri hapo jana
Jumamosi katika mkoa wa al-Anbar, sanjari na kuangamizwa silaha kadhaa
za kundi hilo katika mashambulizi yaliyofanywa kwa kutumia jeshi la
nchikavu.
0 comments:
Post a Comment